lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Maelezo ya Tume
»Sifa za Mbunge
»Sifa za Diwani
»Uteuzi Wagombea
»Mapingamizi
»Kufanya Kampeni
»Upigaji Kura
»Kuhesabu Kura
»Kujumlisha Kura
»Viti Maalum
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Kura za Awali
b.part

Uteuzi wa Wagombea

Siku ya Uteuzi

Siku ya Uteuzi wa Wagombea Urais, Ubunge na Udiwani hupangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Wagombea uchaguzi katika ngazi zote sharti wawe ni wanachama wa Chama cha Siasa na wawe wamependekezwa na Vyama vya Siasa kwa maandishi. Kwa uchaguzi wa mwaka 2005 uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 20 Agosti 2005.

Mamlaka zitakazoshughulikia uteuzi wa wagombea ni kama ifuatavyo:

  1. Mgombea Urais na Umakamu wa Rais - Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  2. Mgombea Ubunge - Msimamizi wa Uchaguzi

  3. Mgombea Udiwani - Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi


Wajibu wa Vyama vya Siasa, Wagombea na Mawakala

Wajibu wa Vyama vya Siasa

  1. Wajibu wa Vyama vya Siasa ni kupendekeza wagombea wa Vyama vyao. Ni vizuri Vyama navyo vijiridhishe kwamba wagombea wanaowapendekeza wanazo sifa zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria. Chama kikishampendekeza mgombea kimpatie mgombea huyo barua ya kumtambulisha rasmi kwa Msimamizi wa Uchaguzi. Vyama ambavyo vina mgawanyiko wa uongozi, vihakikishe kwamba fomu za mgombea wao zinatiwa saini na viongozi wa kitaifa kwa wanaogombea nafasi ya Ubunge na Uongozi wa Mkoa kwa upande wa Wagombea Udiwani ngazi ya Kata. Uongozi wa kitaifa ni ule unaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Wajibu wa Wagombea

  1. Kuhakikisha na kujiridhisha kwamba wanazo sifa zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Uchaguzi, na kwamba hawajaondokewa na sifa yoyote.

  2. Kuelewa barabara aina za fomu zote zinazohitajika kwa uteuzi rasmi; zinapatikana wapi na kwa masharti gani; zinatakiwa kurudishwa lini, wapi na kwa masharti gani. Fomu zinapatikana kwa Msimamizi wa Uchaguzi na zinarudishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi au Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Zile zinazohusu uchaguzi wa Wabunge na Madiwani zinarudishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi na zile zinazohusu uchaguzi wa Rais zinarushwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  3. Kuzielewa haki zao, pamoja na masharti na utaratibu wa uteuzi. Haki hizo ni pamoja na kutoa pingamizi kwa Msimamizi wa Uchaguzi dhidi ya uteuzi wa mgombea yeyote, na kukata rufaa kwa Tume dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kuhusu pingamizi.


Utaratibu wa kushughulikia wapigia kura wanaodhamini mgombea zaidi ya mmoja

Mpiga kura aliyeandikishwa, ataruhusiwa kumdhamini mgombea mmoja kwa kila uchaguzi. Kwa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani mpiga kura mmoja anapodhamini zaidi ya mgombea mmoja kwa kila uchaguzi na wagombea hao wakateuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi, udhamini huo hautabatilisha uteuzi wa wagombea waliodhamini isipokukwa itakuwa ni kosa la jinai kwa mpiga kura aliyedhamini wagombea hao.

Mpiga kura aliyedhamini mgombea zaidi ya mmoja akikubali kosa kwa maandishi, Msimamizi wa Uchaguzi anawaweza kutoa adhabu ya kumtoza faini isiyozidi Shs 200,000/=. Mpiga kura akikataa shauri hilo litapelekekwa Mahakamani na Msimamizi wa Uchaguzi.

Pingamizi dhidi ya Uteuzi wa Wagombea       Soma Zaidi...


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl