Sifa na Masharti ya Mgombea Udiwani
Sifa za mgombea Udiwani
-
Awe raia wa Tanzania
-
Awe na umri usiopungua miaka 21
-
Awe mkazi wa eneo la Halmashauri inayohusika
-
Awe anaweza kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza
-
Awe mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na Chama cha Siasa
-
Awe na kipato halali kinachomwezesha kuishi
-
Awe hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla ya
tarehe ya Uchaguzi
Kupoteza sifa za kuwa mgombea
Hata kama mtu ana sifa zote zilizotajwa hapo juu haruhusiwi kugombea Udiwani kama:-
- Ana uraia wa nchi nyingine
- Amethibitika kisheria kwamba hana akili timamu
- Amehukumiwa kifo na Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania
- Anatumikia hukumu ya kifungo cha zaidi ya miezi sita
- Yumo kizuizini kwa mujibu wa Sheria ya kuwaweka watu kizuizini ya mwaka 1962
- Yuko uhamishoni, kwa zaidi ya miezi sita kwa mujibu wa Sheria ya Uhamishoni (Deportation Ordinance)
- Ni mfanyakazi wa Halmashauri inayohusika au Serikali ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa yule ambaye ameruhusiwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa kifungu cha 40(1)(f) cha Sheria ya Uchaguzi namba 4/79
- Kama amezuiliwa na Sheria yoyote nchini kujiandikisha kuwa mpiga kura
- Ana maslahi katika Halmashauri au Kampuni yenye mkataba na Halmashauri na hajatangaza kwenye gazeti juu ya maslahi
hayo
Masharti ya Uteuzi wa Mgombea Udiwani
- Awe amedhaminiwa na watu wasiopungua kumi walioandikishwa kupiga kura katika Kata.
- Awe amekula kiapo mbele ya hakimu kuthibitisha kwamba anazo sifa zinazotakiwa kugombea Udiwani na kujaziwa fomu ya
uteuzi namba 8C.
- Awe na dhamana ya Shilingi Elfu tano (5,000/=).