lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Maelezo ya Tume
»Sifa za Mbunge
»Sifa za Diwani
»Uteuzi Wagombea
»Mapingamizi
»Kufanya Kampeni
»Upigaji Kura
»Kuhesabu Kura
»Kujumlisha Kura
»Viti Maalum
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Muungano upinzani
b.part

Sifa na Masharti ya Mgombea Ubunge

lf.bevel rt.bevel
Je? Watumishi wa Umma wanaruhusiwa kugombea?
Soma zaidi..
lf.bevel rt.bevel

Sifa za mgombea Ubunge

  1. Awe raia wa Tanzania
  2. Awe na umri wa miaka 21 au zaidi
  3. Awe ni Mwanachama na ni Mgombea iliyependekezwa na Chama cha Siasa
  4. Awe hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi
  5. Awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza


Kupoteza sifa za kuwa mgombea

Kwa mujibu wa Ibara ya 676(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, hata kama mtu ana sifa zote za kugombea hataruhusiwa kugombea Ubunge kama:-

  1. Ni raia wanchi nyingine; au

  2. Kwa mujibu wa Sheria inayotumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa akili; au

  3. Amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au

  4. Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma;

  5. Siyo mwanachama na siyo mgombea aliyependekezwa na Chama cha Siasa;

  6. Ikiwa mtu huyo ana maslahi yoyote katika mkataba wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wa aina yoyote iliyowekewa miiko maalumu kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapo a mekiuka miiko hiyo;

  7. Ameshika madaraka ya Afisa Mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais anaweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, au Sheria iliyotungwa na Bunge;

  8. Kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge inayoshughulikia makosa yanayohusika na Uchaguzi wa aina yoyote, mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha kama mpiga kura au kupiga kura katika Uchaguzi wa Wabunge;

  9. Ni mgombea Urais au Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Masharti ya Mgombea

  1. Awe amedhaminiwa na wapiga kura wasiopungua 25 waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo hilo

  2. Awe na dhamana ya Shilingi Elfu hamsini (50,000/=)

  3. Awe amekula kiapo mbele ya Hakimu kwamba anazo sifa zinazotakiwa ili kugombea Ubunge

Fomu ya Uteuzi wa Mgombea Ubunge       Soma Zaidi...


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl