lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Maelezo ya Tume
»Sifa za Mbunge
»Sifa za Diwani
»Uteuzi Wagombea
»Mapingamizi
»Kufanya Kampeni
»Upigaji Kura
»Kuhesabu Kura
»Kujumlisha Kura
»Viti Maalum
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Kura za Awali
b.part

Pingamizi dhidi ya Uteuzi wa Mgombea Udiwani

Wanaoruhusiwa kutoa pingamizi

  1. Mgombea yeyote wa Kata ya mgombea anayepingwa

  2. Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
Mtu mwingine yeyote haruhusiwi kutoa pingamizi.

Muda wa kutoa pingamizi ni baada ya saa kumi (10.00) jioni ya siku ya Uteuzi mpaka saa kumi (10.00) jioni ya siku inayofuata.

Sababu za Pingamizi

Sababu ya pingamizi inaweza kuwa yoyote kati ya zifuatazo, kwamba:

  1. Maelezo yaliyopo katika fomu ya uteuzi hayatoshi kumtambulisha mgombea;

  2. Fomu ya Uteuzi haitimizi au haikuwasilishwa kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Sheria;

  3. Kutokana na maelezo yaliyoandikwa katika fomu ya uteuzi ni dhahiri kwamba mgombea uchaguzi hana sifa zinazotakiwa;

  4. Uthibitisho wa Msimamizi wa Uchaguzi unaopaswa kutolewa haukutolewa;

  5. Hakuna picha ya mgombea;

  6. Hakuna uthibitisho kuwa mgombea amelipa dhamana shilingi Elfu tano (5,000/=).


Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi

Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi mara baada ya kupokea pingamizi anatakiwa amuarifu kwa maandishi mgombea anayepingwa juu ya pingamizi hiyo na kumtaka atoe maelezo yake juu ya hiyo pingamizi. Mgombea anayepingwa atoe maelezo ya kujibu pingamizi hiyo akipenda kwa Msimamizi wa Uchaguzi mapema iwezekanavyo.

Baada ya kupata taarifa za pande zote Msimammizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi anaweza kuendelea kutoa uamuzi wake. Hata kama anayepingwa hatatoa majibu, Msimamizi wa Uchaguzi anaweza kutoa uamuzi wake.

Rufani Dhidi ya Pingamizi

Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi amwelekeza aliyetoa pingamizi, kukata rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi endapo hakuridhika na uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika muda wa saa 48 tangu kutolewa kwa uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi. Rufaa itawasilishwa kwa kutumia Fomu namba 12.

Uamuzi wa Tume

Uamuzi wa Tume kuhusu rufani utakuwa ni wa mwisho na ambaye hataridhika nao, anaweza baada ya uchaguzi, kufungua malalamiko ya uchaguzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Kipindi cha Kampeni       Soma Zaidi...


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl