|
|
|
|
|
|
Mwaka mmoja tangu kuingia madarakani
Serikali ya CHADEMA ina ahidi kufanya yafuatayo:
Elimu
- Bajeti ya elimu kuongezeka kutoka 18% hadi 35%, kuongeza ajira za waalimu na kuboresha mishahara ya waalimu.
Afya
- Kufuta VAT kwenye huduma na vifaa vya kina mama waja wazito na watoto.
- Madawa ya kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kugawiwa kwa wote walioathirika.
- Kupandisha mishahara ya madaktari na wauguzi.
Kilimo
- Kufuta kodi zote pamoja na VAT kwa pembejeo za kilimo.
- Kuweka mpango thabiti wa kutofautisha ardhi kwa ajili ya umwagiliaji.
Uchumi
- Bajeti 2006/07 kupunguza VAT iwe 16%.
- Kufanya mapitio ya mikataba yote ya uwekezaji na ubinafsishaji.
- Tanzania kujiunga upya na COMESA.
- Kutengeneza ajira milioni moja kwa kufanya mabadiliko makubwa katika sekta za madini, utalii, ujenzi na huduma za
jamii.
Mfumo wa Utawala Bora
- Kurudisha serikalini mali zote zilizochangwa na wananchi na kuhodhiwa na CCM kama viwanja vya mpira na majengo
yanayotumiwa na CCM n.k.
- Kupiga marufuku uuzaji wa nyumba za Serikali na kurejesha zilizokwisha uzwa kiupendeleo.
- Kuvunja PCB na kuweka majukumu yote ya kupigana na rushwa chini ya Mkurugenzi wa makosa ya Jinai (DCI).
- Kuboresha maisha ya kina mama kwa kuwawezesha kielimu na kuwapa nafasi katika utawala.
|
|
|
 |
 |
|
 |
 |
|