lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Maelezo ya Tume
»Sifa za Mbunge
»Sifa za Diwani
»Uteuzi Wagombea
»Mapingamizi
»Kufanya Kampeni
»Upigaji Kura
»Kuhesabu Kura
»Kujumlisha Kura
»Viti Maalum
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Muungano upinzani
b.part


Utoaji wa Fomu za Uteuzi kwa Wagombea Udiwani


  1. Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa fomu chache Makao Makuu ya kila chama cha Siasa kilichopata usajili kamili kwa taarifa.

  2. Wasimamizi wa Uchaguzi watatumiwa fomu kwa ajili ya kuwapa Wagombea. Wagombea watakaopatiwa fomu kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi au Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ni wale tu ambao watawasilisha uthibitisho wa maandishi kwamba wao ndio waliopendekezwa na vyama vyao kugombea udiwani katika Kata inayohusika.

Fomu ya uteuzi namba 8C itatolewa kwa wagombea udiwani ikionyesha:-

  1. Idadi ya wapiga kura waliomdhamini Mgombea
  2. Tamko la kisheria la Mgombea
  3. Maelezo binafsi ya Mgombea
  4. Uthibitisho kuwa amelipa dhamana ya shilingi elfu tano (5,000/=).

Kila Mgombea atapewa nakala nne za kila moja ya fomu hizo.

Akishapatiwa fomu hizo afanye yafuatayo:

  1. Apate watu wasiopungua 10 atakaomdhamini kwa kumjazia nakala nne za Fomu ya uteuzi. Watu hao sharti:-
  1. Wawe wamejiandikisha kuwa wapiga kura katika Kata anayogombea
  2. Wawe hawajamdhamini mgombea mwingine wa Udiwani
  3. Si lazima wawe ni wanachama wa Chama kilichompendekeza; wala si lazima wawe wanachama wa Chama chochote cha siasa.

  1. Aapishwe na hakimu akiwa na nakala zote nne za Fomu ya uteuzi ili kuthibitisha kwamba ana sifa za kugombea udiwani.
  2. Alipe dhamana na shilingi Elfu tano (5,000) fedha taslimu kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

Uwasilishaji wa Fomu ya Uteuzi

Wagombea Uchaguzi wa Udiwani wawasilishe fomu za uteuzi, picha za rangi zenye ukubwa wa 'post card' ("3x4") na dhamana ya shilingi elfu tano (5,000/=) kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika ofisi yake.

  1. Fomu zinaweza kuwasilishwa na mgombea mwenyewe au yeyote kati ya watu 10 waliomdhamini.

  2. Fomu hizo sharti ziwasilishwe kabla ya saa kumi (10.00) jioni ya siku ya Uteuzi.
Dokezo: Mgombea akipenda anaweza kurudisha fomu zake kuanzia siku tatu kabla ya siku ya uteuzi iliyopangwa na Tume lakini uteuzi kamili utafanywa siku ya uteuzi.

Ukaguzi wa Fomu

  1. Msimamizi wa Uchaguzi atazikagua Fomu ya uteuzi pamoja na viambatisho vyake.

  2. Mgombea ahakikishe kwamba nyuma ya picha hizo ameandika jina lake, Kata anayogombea, na chama kilichompendekeza. Jambo hilo ni muhimu sana ili katika karatasi za kura picha ya mgombea 'X' isipewe jina la mgombea 'Y'

Kubandika Fomu ya Uteuzi

Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atabandika kwenye ubao wa matangazo mahali pa wazi nje ya ofisi ya Kata nakala moja moja ya fomu zote na picha ili ziweze kukaguliwa.

Uteuzi wa Wagombea       Soma Zaidi...


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl