lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Maelezo ya Tume
»Sifa za Mbunge
»Sifa za Diwani
»Uteuzi Wagombea
»Mapingamizi
»Kufanya Kampeni
»Upigaji Kura
»Kuhesabu Kura
»Kujumlisha Kura
»Viti Maalum
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Muungano upinzani
b.part


Utoaji wa Fomu za Uteuzi kwa Wagombea Ubunge


  1. Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa fomu chache Makao Makuu ya kila Chama cha Siasa kilichopata usajili kamili kwa taarifa. Fomu hizo zitagongwa muhuri wa sampuli ili zisitumiwe na wagombea.
  2. Wasimamizi wa Uchaguzi wa kila jimbo watatumiwa fomu zitakazotolewa kwa ajili ya wagombea.
  3. Wagombea watakaopata fomu kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi ni wale tu ambao watawasilisha kwake uthibitisho wa maandishi kama wao ndio waliopendekezwa na Vyama vyao vya Siasa kugombea Ubunge wa Jimbo litakalotajwa katika uthibitisho huo.

Kila mgombea atapewa nakala nne za kila moja ya fomu hizo.

Akishapata Fomu:

  1. Apate watu wasiopungua ishirini na tano, watakaokuwa wadhamini wa kumjazia Fomu ya uteuzi.

    Wadhamini hao:

  1. Wawe wamejiandikisha kuwa wapiga kura katika Jimbo analogombea.
  2. Wawe hawajamdhamini mgombea mwingine yeyote.
  3. Si lazima wawe wanachama wa Chama kilichompendekeza, wala si lazima wawe wanachama wa Chama chochote cha siasa.
  1. Ajaze fomu Na. 108 yenye habari zake binafsi, na ahakikishe kwamba habari hizo zinathibitishwa na chama kilichomteua ngazi ya Taifa, Mkoa au Wilaya kwamba ni za kweli.
  2. Awe na nakala nne za picha. Picha hizo ziwe za rangi zenye ukubwa wa 'post card' ("3x4"). Kwa mujibu wa Sheria ni lazima zipigwe katika muda usiozidi miezi mitatu kabla ya siku ya uteuzi.
  3. Siku ya uteuzi alipe dhamana ya shilingi Elfu hamsini (50,000/=) fedha taslimu kwa Msimamizi wa Uchaguzi).

Fomu ya Uteuzi

Mgombea atawasilisha fomu ya uteuzi, dhamana pamoja na picha nne za rangi zenye ukubwa wa 'post card' ("3x4") kwa Msimamizi wa Uchaguzi siku ya uteuzi.

  1. Fomu zinaweza kuwasilishwa na mwenyewe au na yeyote kati ya watu ishirini na tano waliomdhamini.
  2. Fomu hizo sharti ziwasilishwe kwa Msimamizi wa Uchaguzi, siku ya uteuzi, kabla ya saa kumi (10.00) jioni.
  3. Fomu za mgombea ambaye Chama chake kina migogoro katika kuteua mgombea lazima zitiwe saini na uongozi wa kitaifa unaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa. Hii ina maana kuwa fomu za mgombea zinapaswa kutiwa saini na uongozi wa kitaifa wa pande zote zinazohusika.

Dokezo: Mgombea, akipenda, anaweza kurudisha fomu zake kuanzia siku tatu kabla ya siku ya uteuzi lakini uteuzi rasmi utafanyika siku ya uteuzi.

Ukaguzi wa Fomu ya Uteuzi

Msimamizi wa Uchaguzi ataikagua fomu ya Uteuzi kikamilifu.

Mgombea ahakikishe kwamba nyuma ya picha hizo ameandika jina lake, Jimbo analogombea na Chama kilichompendekeza. Jambo hili ni muhimu sana ili katika karatasi za kura picha ya mgombea 'X' isipewe jina la mgombea 'Y'.

Kubandika Fomu ya Uteuzi

Msimamizi wa Uchaguzi atabandika kwenye ubao wa matangazo mahali pa wazi nakala moja moja ya fomu zote na picha za wagombea, baada ya saa saa kumi (10.00) jioni ya siku inayofuata ili ziweze kukaguliwa.

Uteuzi wa Wagombea       Soma Zaidi...


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl