lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2009
»Jiandae kwa 2010
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Gombea Ubunge
»Gombea Udiwani
»Muungano upinzani
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Matamko ya Chama
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
»Katuni
b.part

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2009

lf.bevel rt.bevel
Soma Matokeo ya Uchaguzi wa 2004 wa Serikali za Vijiji, Vitongoji na Mitaa.
lf.bevel rt.bevel

Mwaka 2009 Watanzania tutafanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo tutawachagua viongozi wa vijiji na mitaa. Serikali za mitaa ndio nguzo ya demokrasia katika nchi yeyote duniani, ndio msingi wa mabadiliko katika mchakato wa kulibadili taifa letu.

Hii inatokana na ukweli kuwa ni viongozi wa serikali za mitaa ndio walio karibu na wananchi na kimsingi ni wao walio wa kwanza katika kupanga na kutatua changamoto mbalimbali za wanamtaa na wanakijiji. Na ni wao wanashiriki na kuyaishi matatizo ya wananchi kwa ukaribu zaidi.

Kwa hiyo kama tunataka kuibadili nchi yetu, hatuna budi kukubali kuonyesha hisia na utashi wetu kwa kubadili ushindi katika uchaguzi huo. Ni muhimu sasa kuanza kufikiria namna gani tutapata viongozi mbadala. Wenye fikra mbadala kutoka chama mbadala.

Tukiweza kubadili vijiji vyetu na kuweka viongozi mbadala, Tukiweza kubadili mitaa yetu kwa kuweka viongozi mbadala wa chama mbadala, tutaweza kuibadili nchi yetu. Maendeleo huanzia kwenye familia, familia zenye fikra mbadala hujenga vijiji na mitaa yenye fikra mbadala. Mitaa yenye fikra mbadala hujenga kata, majimbo na hatimaye taifa mbadala.

Hivyo basi, ni jukumu lako wewe uliyeamini juu ya umuhimu wa fikra na uongozi mbadala. Uliyeamini kuwa ni muda muafaka kwa watawala kurejesha uongozi kwa umma kumjulisha jirani yako kuhusu ukweli huo. Ili mwisho wa siku tujenge vijiji na mitaa mbadala kabla ya mwaka 2009 na ifikapo 2009 tusimike uongozi mbadala. , Uongozi utakaojenga vijiji na mitaa tunayoitaka ili mwisho wa siku tujenge majimbo na hatimaye Tanzania tunayoitaka.

Hakuna utawala uliodumu milele isipokuwa wa Mungu, CHADEMA tunaamini kuwa CCM imepoteza uongozi imebaki na utawala. Zama za CCM zimefikia tamati, unyonge wetu umefikia ukomo. Ni muda sasa ewe Baba, ewe mama. Ewe kaka, ewe dada. Ni muda sasa uchukue hatua, shiriki kushawishi Watanzania wazalendo kugombea. Shiriki kugombea mwenyewe ili kwa pamoja tujenge Tanzania tunayoitaka. Tanzania yenye TUMAINI JIPYA!

Jiandae kushiriki Uchaguzi Mkuu 2010       Soma Zaidi...


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl