lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Muungano upinzani
b.part

Maelelezo ya taratibu za Uendeshaji wa Uchaguzi ndani ya chama

Ngazi ya Msingi na Tawi (Katiba ya chama ibara ya 11.1)


II.  Uchaguzi wa Mabalozi

Balozi ni mwakilishi wa chama katika nyumba 10. Mabalozi wa chama watachaguliwa na mkutano mkuu wa msingi (kitongoji/mtaa mdogo).

Uchaguzi wa mabalozi na wa viongozi wa msingi utasimamiwa na viongozi wa tawi, mahali ambapo hakuna viongozi wa tawi, viongozi wa kata watatakiwa kusimamia.

Katika mkutano mkuu wa msingi utakaokaa kwa ajili ya kuchagua viongozi wa ngazi ya msingi utachagua pia mabalozi wa nyumba kumi kumi katika msingi husika. Kwenye eneo la nyumba 10 ambazo hazina mwanachama wa CHADEMA, achaguliwe mtu anayeishi kwenye eneo la karibu na nyumba hizo ili awe mwakilishi wa chama katika nyumba hizo 10 hadi pale atakapopatikana mwana CHADEMA miongoni mwa nyumba hizo 10.


III.  Uchaguzi ngazi ya Msingi (Kitongoji/Mtaa mdogo)

Ngazi ya msingi inafafanuliwa katika katiba ya chama ibara ya 7.1.1 ambayo inasema ifuatavyo: “… Ngazi ya msingi itaundwa katika eneo la kitongoji au mitaa midogo”. Kwa maana hiyo , wanachama wote wa CHADEMA katika kitongoji au mtaa mdogo wataunda msingi mmoja.

Nani anaweza kuunda msingi?

Watu wowote 30 waliohamasika na CHADEMA katika eneo la kitongoji au mtaa mdogo wanaweza kujikusanya na kuanzisha msingi wa CHADEMA katika eneo lao na kuendelea kuhamasisha watu wengine kujiunga na msingi wao.

Viongozi wa ngazi ya msingi

Kiongozi wa ngazi ya msingi wameainishwa katika ibara ya 7.1.3 vifungu (a – f). Viongozi hao ni hawa wafuatao:-

  1. Mwenyekiti wa msingi
  2. Katibu wa msingi
  3. Mabalozi wa nyumba 10 ndani ya msingi
  4. Mwakilishi baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA)
  5. Mwakilishi baraza la wazee
  6. Mwakilishi baraza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA)

Viongozi wa msingi wanachaguliwaje?

Viongozi wa msingi wanachaguliwa kama ifuatavyo:-

  1. Mwenyekiti, katibu na mabalozi wote ndani ya msingi watachaguliwa na mkutano mkuu wa msingi.
  2. Wawakilishi wa mabaraza watachaguliwa na mikutano mikuu ya mabaraza yao ambayo itaketi siku moja na mkutano mkuu wa msingi.

  • Mikutano mkuu wa msingi ni mkutano wa wanachama wote ndani ya kitongoji au mtaa mdogo.
  • Kiingilio katika mkutano mkuu wa msingi au mikutano ya mabaraza ni kadi ya chama au fomu ya uanachama, pia wanachama watakaotaka kujiunga na chama wanaweza kujisajili kwa kujaza fomu kabla ya uchaguzi kuanza.


IV.  Ngazi ya Tawi

Ngazi ya tawi inaundwa kwa mujibu wa katiba ya chama ibara ya 7.2.1 inayosomeka ifuatavyo: “Tawi linaundwa katika eneo la kijiji, mtaa au shehiya ya kiutawala katika mamlaka za serikali za mitaa”. Kwa hiyo wanaCHADEMA waliopo katika misingi mbali mbali ndani ya kijiji, mtaa au shehiya ndio watakaounda tawi.

Viongozi wa ngazi ya tawi

Viongozi wa ngazi ya tawi kama walivyoainishwa katika katiba ya chama ibara 7.2.3 vifungu vya (a – f) ni hawa wafuatao:-

  1. Mwenyekiti wa tawi
  2. Katibu wa tawi
  3. Mweka hazina wa tawi
  4. Katibu mwenezi tawi
  5. Wenyeviti wa mabaraza ya chama ngazi ya tawi
  6. Makatibu wa mabaraza ya chama ngazi ya tawi.

Uchaguzi wa viongozi wa tawi

Uchaguzi wa viongozi wa tawi utaitishwa na kusimamiwa na kata husika. Uchaguzi wa viongozi wa tawi unafanyika kwa mujibu wa ibara ya 7.2.4 ya katiba ambayo inasema “viongozi wa vifungu (a – d) hapo juu watachaguliwa na mkutano mkuu wa tawi na viongozi waliotajwa katika vifungu (e – f) hapo juu watachaguliwa na mikutano mikuu ya mabaraza yao ambayo itafanyika siku moja na mkutano mkuu wa tawi”.

Mkutano mkuu wa tawi

Mkutano mkuu wa tawi ni mkutano wa wanachama wote wa CHADEMA katika kijiji au mtaa au shehiya ya kiutawala.



lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl