28 Novemba 2007
Tamko kuhusu kuundwa kwa Kamati ya Uchunguzi wa Mikataba ya Madini
Kamati Kuu inamtaka Rais kutoa hadharani na/au kwa wawakilishi wa kuchaguliwa wa wananchi Ripoti za Kamati za Uchunguzi zilizokwisha kuundwa na serikali kuchunguza matatizo mbalimbali ya madini ikiwemo Kamati ya Jenerali Mboma (2001), Kamati ya Brigedia Jenerali Mang’enya (2003), Kamati ya Dr. Kipokola (2004) na Kamati ya Masha (2006)...
15 Oktoba 2007
Tamko kuhusu kauli potofu ya Kingunge
Waziri Kingunge anaupotosha umma anaposema kwamba ziara za viongozi wa upinzani zinatokana na ‘hasira ya kushindwa uchaguzi mkuu 2005, kambi ya upinzani kushindwa kumtetea Zitto bungeni, wivu wa kuona CCM inatekeleza ilani yake vizuri, na kwamba wanautumia vibaya mfumo wa vyama vingi’...
14 Oktoba 2007
Tamko la CHADEMA kuhusu ufafanuzi wa Serikali juu ya tuhuma za ufisadi
Itakumbukwa kwamba Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo walitoa kile walichoita tamko ama ufafanuzi juu ya tuhuma za rushwa na ufisadi zinazoendelea hapa nchini na kama zilivyoibuliwa na Mbunge wa Karatu - Dkt. Willbroad Slaa kupitia ‘orodha ya mafisadi’ (list of shame) aliyoitoa hadharani....
14 Mei 2007
Tamko la Wakuu wa Vyama Juu ya Ushirikiano wa Vyama vya Siasa
Sisi viongozi wa vyama vya siasa vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), The Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi), National Convention for Construction and Reform (NCCR - Mageuzi) na Tanzania Labour Party (TLP) tuliokaa Dar es Salaam leo hii tarehe 10 Mei 2007...
1 Desemba 2006
Tamko la Baraza Kuu la CHADEMA kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2005
Sisi, wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA tumetathmini na kujadili kwa kina Uchaguzi Mkuu wa 2005 na kwa pamoja tumeazimia kutoa tamko hili linaolotoa msimamo wa CHADEMA kuhusu mapungufu, mafanikio, mapendekezo na mwelekeo kuhusu uchaguzi husika...
29 Mei 2007
Tamko la Vijana kuhusu Wanafunzi wa Ukraine waliotelekezwa na Serikali
Tulitegemea Waziri mwenye dhamana ya wizara hii angejitokeza sasa kutoa ufafanuzi kuhusu suala zima. Hii ni ishara ya kukosa uwajibikaji. Sijui Waziri Msolla anafanya kazi ya kuwatumikia walipa kodi wa nchi gani kama masuala yanayowahusu Watanzania yanayoigusa wizara yake anakwepa kutolea ufafanuzi...
6 Januari 2007
Shutuma hizi kwa CHADEMA na Freeman Mbowe si za kweli
Mwishoni mwaka 2006 na mwanzoni mwaka huu shutuma kadhaa zimeelekezwa kwa CHADEMA na viongozi wake hususani Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Mwanzoni shutuma hizi zimekuwa zikitolewa na wanasiasa wanaojitoa kambi ya upinzani na kujiunga na CCM...
29 Disemba 2006
CCM haiwezi kupambana na Rushwa ndani ya chama chao
Chama Cha Mapinduzi CCM, kimedai kuzindua utaratibu wa kupambana na rushwa ndani ya chama chao kwa kutenga siku maalumu ya kuzungumzia rushwa katika ngazi ya shina mpaka taifa...
5 Disemba 2006
Waziri Chiligati amewapotosha Vijana na Watanzania
Si kweli kwamba karibu asilimia 60 ya mabaraza ya madiwani ni vijana.
Si kweli kwamba katika bunge la Tanzania kuna wabunge vijana 30.
Si kweli kuwa wabunge vijana ni asilimia 10 ya wabunge wote...
23 Novemba 2006
Taarifa kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu walionyimwa mikopo na Serikali
Vijana wa CHADEMA tunatoa mwito kwa vijana wote ambao kwa namna mmoja au nyingine walitapeliwa na serikali kuwasilisha malalamiko yao CHADEMA kwa ajili ya kuanza ufuatiliaji...
17 Novemba 2006
Tamko kuhusu uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki
Tamko hili linatoa taarifa ya timu ya kampeni ya mgombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu mapungufu, mafanikio, mapendekezo na mwelekeo kuhusiana na mchakato wa uchaguzi husika...
28 Oktoba 2006
Tamko la vijana wa CHADEMA kuhusu mwelekeo wa Taifa na Chama
Tunaongozwa na hiari na utashi wetu kutoa tamko hili, tunashawishiwa na umakini wetu kutetea vijana wa nchi hii, na tunashinikizwa na uzalendo wetu kwa taifa letu kuwajibika namna hii...
6 Oktoba 2006
Wanawake CHADEMA waungana na Wanaharakati kumkosoa Mama Kikwete
“Nimeamua nitoe tamko kwa niaba ya wanawake wa CHADEMA kuhusu suala hili baada ya kuona kuwa wanaharakati wanashambuliwa sana kwenye vyombo vya habari kupitia makala mbalimbali kuhusu suala hili. Napata hisia kwamba kuna mkakati wa kumsafisha na kumtetea mke wa rais"...
28 Septemba 2006
Makamba acha kupotosha Watanzania
CHADEMA kinapenda kutoa tamko kufuatia kauli ya upotoshaji iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Mh Luteni Yusuph Makamba wiki jana alipokuwa katika ziara yake ya kampeni wilayani Karatu ambapo alikuwa akihamasisha Watanzania waliopo Karatu wajiunge na CCM...
24 Septemba 2006
CHADEMA yaiomba TFF ishirikishe wadau wengine Kamati ya Stars
Awali ya yote CHADEMA tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa kazi nzuri walioifanya kuhakikisha wanaifunga timu ya Bokina faso siku ile ya Septemba2, 2006. CHADEMA tunaamini kuwa ulikuwa mwanzo mzuri na kwamba uwezo wa kushinda zaidi tunao...
3 Juni 2006
Tamko la Kurugenzi ya Vijana kuhusu kauli ya UVCCM
Bwana Makala katika hotuba yake aliyoitoa wilayani Temeke, alidai kuwa “Mbowe alitoa kauli kuwa rais Kikwete amekuwa ni mtu wa kutoa ahadi, kuzunguka na kutokaa ofisini”. Makala alidai kuwa “Kikwete anafanya hivyo kuonyesha kuwa anawajali wananchi na matatizo yao na ndio maana anazunguka ili ajue na kufanya utafiti na sio kukaa ofisini na kusubiri matatizo”...
7 Mei 2006
Siku 100 za utawala wa Kikwete
Kauli mbiu ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya imeleta mwamko mpya wa kiutendaji. Rais amefanikiwa katika hotuba zake mbalimbali hususani hotuba ya kufungua bunge, kukiri mapungufu ya msingi ambayo CHADEMA na wadau wengine wamekuwa wakiyataja kama masuala yanayolikwaza taifa...
2 Mei 2006
Tamko la chama kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2005
Tumetathmini na kujadili kwa kina uchaguzi husika na kwa pamoja tumeazimia kutoa tamko hili linaolotoa msimamo wa CHADEMA kuhusu mapungufu, mafanikio, mapendekezo na mwelekeo kuhusu uchaguzi mkuu 2005. Tunaamini tamko hili litakuwa changamoto kwa wanaCHADEMA...
|