lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matokeo Kiteto 2008
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Tamko la Uchaguzi wa Kiteto

VII. Ushiriki wa Vyombo vya Habari

Vyombo vya habari vimeweza kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha uchaguzi huu na ni wazi kuwa vimeonesha ukomavu mkubwa katika kutoa taarifa zao. Tunavipogeza kwa hilo ingawa changamoto imekuwa ni muda ambao vyombo vya habari vinafika maeneo ya uchaguzi. Ni wazi kuwa waandishi walifika Kiteto nyakati za mwisho wa kampeni badala ya kuwepo tangu mwanzo wa mchakato hali iliyosababisha Umma kutofahamu baadhi ya mapungufu yalijitokeza tangu mchakato wa kampeni ulipoanza. Rai yetu ni kuvitaka vyombo vya habari vizidi kuyapa umihimu mkubwa masuala ya uchaguzi kwa kushiriki kila hatua ili kuongeza ufanisi katika zoezi zima la uchaguzi.

VIII. Msimamo wa CHADEMA kuhusu mchakato mzima wa Uchaguzi

Kufuatia mwenendo mzima wa uchaguzi Kiteto na Mwelekeo wa Taifa kwa ujumla CHADEMA tunachukua hatua zifuatazo;
  1. Kuhusu Viongozi waliopigwa

    Tunaitaka serikali ifikishe suala hili mahakamani haraka iwezekanavyo. Na endapo watachelewa tutaisimamia wenyewe.

    Na kwa kuwa IGP Said Mwema alitangaza kuunda kikosi cha uchunguzi wa kadhia hii tunamtaka aweke wazi matokeo ya tume aliyounda kufuatia vurugu na kupigwa kwa viongozi wa CHADEMA. Hasa kwa kuwa moja ya silaha zilizotumiwa ni kemikali ambayo mpaka sasa haijajulikana.

    Lakini pia tunasikitika kwamba mpaka sasa wadau wa Demokrasia nchini kama wanaharakati wa haki za binadamu, viongozi wa dini na wadau mbalimbali wameonekana kutojali unyama waliofanyiwa viongozi wa CHADEMA , unyama ambao unaweza kupelekea machafuko ya kisiasa katika nchi yetu.

  2. Kuhusu CCM kuvamia mikutano ya CHADEMA

    Tunapenda kuwafahamisha Watanzania kuwa tumekwisha fungua kesi polisi Kijungu na mpaka sasa hatujui polisi inasubiri nini kumkamata Mkurugenzi wa TOT, Mh Komba. Lakini zaidi tunashangaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijaeleza lolote kuhusu uvunjaji wa taratibu za uchaguzi wa makusudi kwa kiwango hiki. Tunaitaka serikali ichukue hatua haraka kabla hatujachukua hatua wenyewe kwakuwa hatuwezi kukubali suala hili liishe kirahisi. Tunavipongeza vyombo vya habari kwa namna walivyolipa uzito suala hili.

  3. Matumizi ya fedha za Kampeni

    CHADEMA tumekuwa na utamaduni wa kuweka waazi matumizi yetu ya fedha za kampeni kwa lengo la kushinikiza mfumo wazi wa matumizi ya fedha za kampeni.

    Tunarudia tena kuitaka serikali kutunga sheria ya lazima kuwepo mipaka ya matumizi ya fedha katika kampeni na uwazi katika matumizi ya fedha za kampeni. Ufisadi unaoliangamiza taifa hili ni matokeo ya matumizi makubwa ya fedha katika kampeni kiasi cha kusababisha pesa kushinda sera katika uchaguzi.

    Kwa msingi huo tunapenda kuwataarifu watanzania kuwa CHADEMA katika uchaguzi huu tumetumia shilingi milioni 48, milioni 15 ikiwa ni mchango wa chama na milioni 33 ikiwa ni michango ya wanachama. Lakini kwa taarifa tulizonazo, CCM imetumia zaidi ya bilioni 1 katika uchaguzi mdogo wa Kiteto huku sehemu kubwa ikitumika kutoa rushwa. Kwa mfano; CCM ilimnunua kijana Omari wa kata ya Matuti kwa shilingi milioni 2. Na ikamlipa Mwenyekiti wa CHADEMA kijiji cha mbigiri baiskeli na shilingi laki 5 ili aingie CCM. Wakati huo huo ilikuwa na magari si chini ya 50, pikipiki, na walikuja na fuso imejaa baiskeli mpya.

rudi...     inaendelea...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl