lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matokeo Kiteto 2008
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Tamko la Uchaguzi wa Kiteto

III. Ushiriki wa Jeshi la Polisi

Jeshi la polisi lilikuwa mihimili muhimu sana kwa ushindi wa CCM Kiteto. Polisi wa Kiteto walifanya kazi pamoja na CCM kuidhibiti CHADEMA kwa kutumia mabavu na kila aina ya mizengwe kwa faida ya CCM. Matukio ya uvunjifu wa amani yalifanywa mbele ya polisi na hata tulifipokisha malalamiko rasmi polisi, polisi walihofu kuchukua hatua stahiki na pale walipoona aibu walijitahidi kuwabembeleza viongozi wa CCM badala ya kuchukua hatua kama chombo cha dola. Kwa mfano;

  1. Maafisa wa Uhamiaji walimzuia uwanja wa ndege Dodoma fundi wa helikopta yetu kwa zaidi ya saa mawili bila kumweleza sababu za msingi.
  2. CCM kwa kuwatumia makomandoo wake walivamia mkutano wa Kijungu na kuwapiga raia na kuwajeruhi mbele ya polisi lakini polisi hawakuchukua hatua zozote hata baada ya vyombo vya habari kuripoti unyama huo.
  3. Kata ya Matui polisi walielezwa kuwa waziri wa viwanda na biashara alikuwa akiendesha zoezi la kununua shahada za kura lakini hawakukubali kwenda kuzuia zoezi hilo.

IV. Ushiriki wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Tumezungumza kwa muda mrefu sasa kuwa mfumo wa Tume ya Uchaguzi tulionao unaifanya tume wakati wote kufanya kazi za chama tawala badala ya kuwa mwamuzi. Katika uchaguzi wa Kiteto baadhi ya matukio yaliyojitokeza kuthibitisha ubutu wa tume yetu ya uchaguzi ni kama yafuatayo;
  1. Katika maeneo ambayo CHADEMA kilikuwa na nguvu kubwa kama Olkery mbugani ambako wananchi walikuwa na hasira dhidi ya CCM kwa kuchomewa nyumba zao, Tume ilihamisha vituo vya kupiga kura hadi Loltepes shuleni umbali wa hadi kilimoita 13 bila taarifa ya wazi isipokuwa kwa CCM ambao mara moja tuliwaona wakiwasomba watu wao kwenye malori wakiwapeleka eneo jipya vilipohamishiwa vituo.
  2. Katika kata ya Matui, walimu wa shule ya msingi ambao walikuwa wasimamizi wa vituo vya uchaguzi walikuwa wapiga debe wa CCM, walivaa sare za CCM, waliwapikia chakula viongozi wa CCM, na waliendesha kampeni za CCM katika eneo hilo. Hata baada ya kuiandikia tume barua kueleza kuwa hatukuwa na imani na wasimamizi 11 wa vituo hivyo, tume ya uchaguzi haikuchukua hatua.Hata mwalimu Musa wa shule ya msingi ya hostet aliyekuwa mpiga debe wa CCM na aliyeshiriki harakati za CCM akiwa mstari wa mbele bado aliruhusiwa kuwa msimamizi wa kituo.
  3. Watendaji wa kata ambao pia ni wasimamizi wa uchaguzi walishiriki kampeni za CCM ikiwa ni pamoja na ofisi zao kutumika kwa shughuli za CCM kufanya vikao wakati wa kampeni.
rudi...     inaendelea...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl