lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matokeo Kiteto 2008
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Tamko la Uchaguzi wa Kiteto

I. Utangulizi

Itakumbukwa kuwa Februari 24, 2008 Watanzania wa Kiteto walihitimisha mchakato muhimu katika ujenzi wa demokrasia kwa kufanikisha mchakato wa uchaguzi uliochukua zaidi ya mwezi mmoja wa kampeni na mivutano mikubwa ya kisiasa na hata kisheria kuhusu mwenendo mzima wa namna ambavyo uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Ikiwa ni takribani wiki moja sasa tangu kumalizika kwa uchaguzi na kukamilisha mchakato wa kufanya tathimini ya Uchaguzi tunadhani ni muda muafaka kuwaeleza wananchi kwa kina kile kilichotokea katika uchaguzi wa Kiteto kwa lengo la kuzidi kuimarisha demokrasia nchini tukiamini kuwa ni mifumo ya kidemokrasia pekee inayoweza kulinusuru Taifa hili dhidi ya Umasikini na Ufisadi unaozidi kuhatarisha amani ya nchi yetu.

Mtakumbuka kuwa CHADEMA kwa niaba ya kambi ya upinzani kilimsimamisha Victo Kimesera, mgombea ambaye kwa uchunguzi wa vyombo huru vya habari ndiye aliyekuwa anapewa nafasi kubwa ya ushindi ingawa hata hivyo matokeo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi hayakuweza kuakisi ukweli huo.

Kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla na wanaCHADEMA tunatoa tamko hili baada ya kufanya tathimini ya kina tukiamini kuwa mafunzo yanayopatikana katika uchaguzi wa kiteto ni changamoto kwa demokrasia ya nchi yetu hivyo kama wadau wa demokrasia ni muhimu kuwashirikisha wadau wengine na Umma wa Watanzani kwa ujumla juu ya kile kilichotokea ili hatua muhimu zichukuliwe kuhakikisha demokrasia katika nchi yetu.

II. Ushiriki wa Wananchi na Vyama vya Siasa

Tunapenda kushukuru kuwa katika zoezi zima la uendeshaji wa kampeni CHADEMA tumeweza kuwa wavumilivu kwa kuendesha kampeni za hoja. Tuliweza kuwafikia wananchi wote na kuwapa ujumbe wa ukombozi, na niwazi kuwa sehemu kubwa ya Umma iliamua kutuunga mkono kwa hoja na mikakati dhahiri ya kisayansi isiyokuwa na ghiliba, matusi, Uongo wala rushwa kama ilivokuwa ikifanywa na CCM.

Ni kwa fursa hii tunawapongeza wananchi wa kiteto walio onesha ujasiri kushinda vitisho, vipigo, rushwa, ghiliba na kila aina ya uzandiki na unyama uliokuwa ukiendeshwa na CCM wakishirikiana na polisi pamoja na watendaji wa vijiji, Kata, Mkuu wa wilaya wa Kiteto na wakuu wa mikoa wa Manyara na Iringa. CHADEMA tunaamini wanakiteto hawatakata tamaa wala kurudi nyuma katika harakati za kusaka mabadiliko na badala yake watachukulia matokeo haya kuwa Changamoto ya kuendeleza mapambano kusaka mabadiliko kwakuwa yanawezekana.

CHADEMA tunaamini kuwa asilimia 53 ya wananchi ambao hawakupiga kura ni aibu kwa serikali makini hasa katika mazingira ambayo kuna kila ushahidi kuwa wananchi wamezuiwa kushiriki mchakato wa upigaji kura kwa nguvu za ghiliba, ufisadi na uzandiki. Tunaitaka serikali ichukue hatua kudhibiti mwenendo wa wimbi hili kwa kuwa mwenendo huu unaashiria ufinyu wa demokrasia na unahatarisha uhalali wa serikali inayotawala.

Moja ya matatizo makubwa yaliyochangia mbinu chafu za CCM kufanikiwa ni pamoja na kutumia fursa ya idadi kubwa ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika (asilimia77 ya wakazi wa Kiteto hawajui kusoma na kuandika) Hali ni mbaya zaidi maeneo ya mashambani Ambapo wengi walijikuta kura zao zikielekezwa kwa mgombea wasiye mtaka na matukio kadhaa ya mivutano kati ya wasiojua kusoma na wasimamizi ilijitokeza lakini wasimamizi wa uchaguzi hawakuzingatia malalamiko hayo hata pale mwananchi husika alipolalamika baada ya kugundua kuwa kura yake imewekwa kwenye picha ya mgombea asiyemtaka.

Aidha ufukara wa wananchi hasa katika majira haya ambapo wananchi wanasubiri kuvuna mazao ilichangia kwa sehemu kubwa mkakati wa CCM kununua shahada za kupigia kura. CHADEMA tulijitahidi kukabiliana na uchafu huu na tuliweza kuripoti matukio kadhaa polisi, TAKUKURU na hata kwenye vyombo vya Habari na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ingawa haikuweza kusaidia sana kwasababu vyombo husika vilishindwa kuchukua hatua dhidi ya wahusika kuweza kukomesha mwenendo huo. Hivyo matokeo kuwa asilimia 53 haikujitokeza kupiga kura ni kielelezo cha mchezo huo mchafu wa ununuzi wa shahada za wapiga kura.

Hata hivyo, pamoja na mchezo mchafu wa CCM kuhakikisha maeneo ya miji ambayo yana wapiga kura wengi na ambayo CHADEMA ina nguvu kubwa wananchi hawajitokezi kupiga kwa kuendesha mradi mkubwa wa kununua shahada mbele ya TAKUKURU, polisi na viongozi wa serikali na kufanya idadi ya waliojitokeza kupiga kuwa kuwa kati ya asilimia20 mpaka 30, bado CHADEMA tulishinda kwa asilimia 71 ikiwa ni pamoja na makao makuu ya wilaya.

Ni wazi kuwa CCM ilichafua mwenendo mzima wa kampeni kwa ukiukaji mkubwa wa sheria, taratibu na kanuni kwa kutumia michezo michafu. Hawakuwa na hoja, walijielekeza zaidi katika kampeni za kejeli, ghiliba, vurugu na matusi mambo ambayo ni aibu kwa taifa letu.

Lakini pia uchaguzi huu umeweka wazi unafiki uliokuwa ukifanywa na CCM kudai kuwa CHADEMA inafanya matumizi mabaya kwa kutumia helkopta kwa kujua kuwa helikopta ilikuwa mwiba kwao. Ni wazi CCM wamejiabisha kwa kutumia helikopta ilhali walizunguka nchi nzima kudanganya Umma kuwa wao wasingeweza kutumia helikopta kwa uzushi kuwa ni gharama kubwa. CHADEMA tutaendelea kuibua mbinu zaidi za kisayansi katika kuendesha siasa za nchi hii tunawakaribisha waendelee kujifunza kutoka kwetu. Kinachosikitisha tu ni kwamba badala ya CCM kuiga sera makini za CHADEMA ili kuboresha maisha ya watu, wanaiba mikakati ya kampeni za CHADEMA.

    inaendelea...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl