Waziri Magufuli ingilia kati hatma ya wakazi Kibamba
- Utekelezaji wa mradi wa Miundo Mbinu ya ngazi ya wilaya eneo la Luguruni na Kibamba Hospitali kukiuka sheria za ardhi za Tanzania na haki za makazi
- Maofisa wanaotuhumiwa kujihusisha na rushwa na kuvunja haki za binadamu katika utekelezaji wa mradi wachukuliwe hatua
- Mchakato wa mradi uwekwe wazi kwa Umma
Kwa tamko hili naungana na wakazi wenzangu wa Jimbo La Ubungo wanaokaa katika Kata ya Kibamba kupinga kitendo cha kutaka kuwahamisha Kimabavu kutoka katika ardhi na makazi yao ambavyo wamemiliki kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi ya Tanzania kwa kushirikisha ngazi zote za Serikali ya Muungano wa Tanzania zikiwemo Serikali za Vijiji, Mitaa, Kata, Manispaa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. Kuwahamisha Kimabavu ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria za Ardhi pamoja na Haki za Makazi kama zilivyoainishwa katika Tamko la Kimataifa ya Haki za Binadamu, ambayo Tanzania imesaini.
Kwa hakika, vitendo vya watumishi wa Wizara yako, Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni waliokabidhiwa jukumu la kutekeleza mradi huu vimepelekea utekelezaji wa mradi huu kuchukua sura ya kuhamisha watu kimabavu kutokana na kukiuka kabisa mwongozo wa uhamishaji watu kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Haki za Makazi; mikataba ambayo Tanzania imeridhia. Na baada ya kuridhia Serikali ya Tanzania iliwajibika kuuingiza mwongozo huo katika Sheria za Ardhi zinazoongoza watu kuhamishwa kutoka katika Ardhi na Makazi yao.
Hivyo basi namuomba Mhe John Magufuli- Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi kuingilia kati suala la wananchi wa Jimbo la Ubungo Kata ya Kibamba kuhamishwa kimabavu katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundo mbinu eneo la Luguruni na Kibamba Hospitali na kufanya yafuatayo:-
Imetolewa 16 Januari 2008 na:
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa(CHADEMA) na Mkazi wa Jimbo la Ubungo