lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Ujumbe wa Vijana wa CHADEMA kuunga kuhusu BAVITA

Vijana na watanzania wamengoja sana kuhusu baraza la vijana. Suala hili lilijiotokeza katika kikao cha bunge la Februari 2006 kutokana na swali la Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA). Lakini majibu aliyoyatoa naibu waziri, Mheshimiwa Daniel Nswanzugwako bado yaliacha maswali na maswali mengine zaidi yamezuka kutokana na hotuba ya bajeti ya wizara katika kikao cha bunge la bajeti ya 2006/07. Maswali haya yanapaswa kujadiliwa wakati Bunge likiwa katika kikao cha bajeti ya 2007/08 huku bajeti ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana ikiwa imepangwa kusomwa na kupitishwa tarehe 1 Agosti 2007.

Tuanze kwa  kusema kwa miaka kumi sasa baraza limekuwa ahadi. Litaendelea kuwa ahadi mpaka lini? Itakumbukwa kwamba hitaji ya kuwa na baraza la vijana la taifa lilijitokeza pindi Tanzania tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Katika hali hiyo umoja wa vijana wa chama tawala ukakosa uhalali wa kuwaratibu vijana wote nchini na kuwawakilisha katika matukio na michakato ya kitaifa na kimataifa. Vijana wakagawanyika kiitikadi. Pindi ikaonekana haja ya kuwa na chombo cha kuwaunganisha vijana wote na kuchochea maendeleo yao. Vuguvugu hili likaanza kukolea mwaka 1996 vijana walipoazimia kuanzisha baraza wenyewe na likashika kasi zaidi mwaka 1997 chini ya utaratibu wa asasi ya vijana ya National Youth Forum(NYF) ambayo baadaye asasi hii ilifutiwa na usajili na serikali.

Serikali iliamua kuingilia kati, ‘ikateka’ ajenda na kuitisha Kongamamo la Vijana Iringa mwaka 1998, huu ndio ulikuwa mwanzo wa mchakato rasmi(official take of point) ya uanzishwaji wa baraza. Katika mkutano huu, rasimu mbalimbali ziliwasilishwa hatimaye mkutano ukakubaliana katika rasimu moja ya kuongoza mjadala. Kongamano hili likaunda kamati ya taifa ya vijana iliyokuwa na uwakilishi wa vijana wa kada mbalimbali. Kamati hii ikapewa hadidu rejea kubwa mbili: Mosi, kuzunguka kukusanya maoni ya vijana kuhusu rasimu ya awali na kuandaa rasimu ya mwisho ya katiba ya baraza. Tatu; kuitisha kongamano lingine la Taifa la vijana kupitia rasimu hiyo kabla haijawasilishwa serikalini. Ili hatua zingine za uandaaji wa muswada kwa ajili ya kwenda bungeni zifuate. Kutoka 1998 suala la baraza limekuwa ni ahadi ya kila mwaka, serikali ya awamu ya tatu imekuwa kila wakati ikisema muswada uko katika hatua za mwisho za kuletwa bungeni lakini hilo halitokei. Je, ile kamati ya Iringa bado ipo hai?Si ajabu kukuta wajumbe wake wengi tayari wameshavuka umri wa ujana kutokana na ngoja ngoja ya miaka mingi.

Bajeti ya mwaka 2006/07, imeonyesha kwamba serikali ya awamu ya nne nayo inaelekea kuendeleza utamaduni huo. Jibu la naibu mwanzoni mwa mwaka Februari 2006 ni kwamba baraza litaundwa hivi karibuni. Hakukuwa  fungu bayana lililotengwa katika bajeti ya wizara kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa uanzishwaji wa baraza la vijana la Taifa katika bajeti iliyopitishwa bajeti husika na kupelekea mwaka mmoja kupita toka ahadi ya waziri ilipotolewa bila ya baraza kuundwa. Kama katika bajeti za wizara  zilitengwa pesa kwa ajili ya uanzishwaji wa tume na mabaraza mbalimbali vipi hatujajipanga kwa ajili ya baraza la vijana? Kama halitatengwa fungu katika bajeti ya Wizara husika ya mwaka wa fedha 2007/08 tafsiri ni kwamba mchakato wa kuunda baraza hautakamilika katika mwaka mzima unaofuata pia. Vijana wasubiri mpaka lini? Serikali itoe ufafanuzi kuhusu suala hili.

Kwa upande mwingine, serikali inapaswa kuzingatia hadidu rejea za Iringa katika kukamilisha mchakato kuundwa kwa baraza huru la taifa la vijana. Kwa kuanzisha baraza hili, serikali yetu itakuwa imetekeleza makubaliano ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa na umoja wa Afrika kuhusu Vijana ambayo nchi yetu imeridhia. Chombo hiki kitakuwa mhimili muhimu katika utekelezaji wa sera ya maendeleo ya vijana Tanzania na kuwa chombo cha kuwaunganisha vijana katika hekaheka zao za kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Pia tunachukua fursa hii kuitaka Wizara inayohusika kuwasilisha Bungeni Mkataba wa Vijana wa Afrika(African Youth Charter) ambao nchi yetu imetia saini toka mwaka jana ili uweze kuridhiwa(ractified); mkataba huu pamoja na mambo mengine unaziwajibisha serikali za Afrika kuanzisha mabaraza ya vijana.

Kwa upande wetu CHADEMA tumeshaifanyia mabadiliko katiba ya chama chetu mwaka 2006 kwa kuruhusu uanzishwaji wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA). Uamuzi wa kuunda Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya vijana ya CHADEMA. Ni sehemu ya mwendelezo wa jitihada za chama za kutoa fursa kwa vijana kama chama mbadala kinachotambua mchango wa kizazi kipya katika kuchochea demokrasia na maendeleo. Uamuzi huu unalenga pia kutekeleza sera za kimataifa kuhusu vijana mathalani Mkakati wa vijana wa Dakar na Mpango wa vijana wa dunia kuanzia mwaka 2000 na kuendelea. Kwa upande mwingine msukumo ziada wa kuunda baraza la vijana kutokana na uzoefu wetu hususani katika uchaguzi mkuu 2005 kama vijana wa CHADEMA wa haja ya kuwa na chombo kipana zaidi cha kuwaunganisha vijana pamoja.

Pamoja na malengo na majukumu ya kisiasa kwa kuwa BAVICHA ni baraza la chama cha siasa, baraza la vijana wa CHADEMA lina wajibu wa kutetea maendeleo ya vijana ikiwemo kuwasadia vijana wenye matatizo, kuunga mkono harakati makini za vijana na kushirikiana na vijana wa sekta mbalimbali. Wajibu huu ni muhimu sana hususani katika wakati wa sasa ambapo jumuia nyingi za vijana zipo kimya kutetea maslahi ya vijana na kuwahamasisha kutimiza wajibu wao. Pia BAVICHA linahamasisha vijana wa CHADEMA kushiriki shughuli za kisiasa na kijamii ikiwemo kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya michezo/kiuchumi na kudhibiti madawa la kulevya na UKIMWIVVU.

Ni imani yetu uamuzi wa kuunda Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) utatoa changamoto kwa serekali kuharakisha mchakato wa uundwaji wa Baraza la Vijana la Taifa (BAVITA). Sisi vijana wa CHADEMA tunaunga mkono uanzishwaji wa baraza la vijana la Taifa ambalo litaunganisha vijana wote wa Tanzania bila kujali itikadi. Umoja ambao uliwekewa ufa baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi na hivyo umoja wa vijana wa chama tawala kupoteza uhalali wa kuwa kiungo na kiwakikilishi cha vijana wote. Lakini katika mchakato huu lazima ukamilishwe kwa kuzingatia matakwa ya vijana.

Kwa vyovyote vile baraza la Taifa (BAVITA) lazima liwe na uanachama mpana na wa aina mbalimbali utakaowakilisha maslahi ya vijana wa sekta mbalimbali. Kwa upande mwingine pamoja na kupata ruzuku serekalini kama ilivyo katika nchi nyingine ni vyema baraza likawa na uwezo wa kupata raslimali toka kwa wanachama wake na wadau wengine ili kuliepusha kupoteza uhuru wake kutokana na utegemezi. Kwa upande mwingine viongozi ni vyema wakatokana na vijana wenyewe kupitia mchakato wa kidemokrasia na watendaji wapatikane kupitia mfumo wa wazi wenye ushindani.

Umetolewa na:

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl