lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

UTANGULIZI

Mwishoni mwaka 2006 na mwanzoni mwaka huu shutuma kadhaa zimeelekezwa kwa CHADEMA na viongozi wake hususani Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Mwanzoni shutuma hizi zimekuwa zikitolewa na wanasiasa wanaojitoa kambi ya upinzani na kujiunga na CCM.

Shutuma hizi ni pamoja na:

  1. Kuwa CHADEMA awali kilianzishwa wakati wa ukoloni kikijulikana kama Chagga Development Manifesto (CHADEMA) ambacho bado kinaendelea na mwelekeo huo (Rejea Majira: 24/12/2006).

  2. CHADEMA ina mrundikano wa watu wa kabila la wachagga. Haipaswi kuwa ‘chama cha demokrasia na maendeleo’ badala yake inapaswa kuitwa “chagga development manifesto” Rejea Mwananchi: 24/12/2006. (Hoja hii ilirudiwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wiki kadhaa mfululizo wakinukuliwa viongozi wachache waliojitoa kutoka upinzani).

Awali CHADEMA tulipuuza uzushi huu. Lakini kutokana na kauli hizi kurudiwa rudiwa mara kwa mara tunaamini kuwa uwongo na upotoshaji huu unaweza kugeuzwa na umma watanzania ukaaminishwa kuwa ndio ukweli.

Aidha, tunatoa taarifa hii kufuatia taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Aggrey Mwanri iliyochapwa katika vyombo mbalimbali vya habari 5 Januari 2007 ambapo CCM imetoa shutuma kadhaa kwa CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.

Pia taarifa hii imetolewa kujibu shutuma kadhaa zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kupitia maoni ya Mhariri wa gazeti la Mtanzania la tarehe 5 Januari 2007 yaliyokuwa na kichwa cha habari “Wapinzani tafuteni njia bora za kukubalika”.

  inaendelea...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl