lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Ushindi wa Kishindo au Ufisadi wa Kishindo?


II.  TANGOLD LIMITED

Kama Orodha ya Mafisadi inavyoonyesha, Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni inayomilikiwa na baadhi ya Mafisadi tuliowataja katika Orodha hiyo. Kuna utata mkubwa zaidi ambao umeigubika kampuni ya Tangold Ltd. Kwanza, licha ya nyaraka kuonyesha kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006, nyaraka za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba Tangold Ltd. ilifungua akaunti ya shilingi Na. 011103024852 NBC Corporate Branch tarehe 1 Januari 2003. Kama ilivyokuwa kwa Deep Green Finance, siku ya Tangold Ltd. kufungua akaunti yake NBC ilikuwa ni Siku ya Mwaka Mpya na siku ya mapumziko kote nchini! Aidha taratibu za kibenki za ufunguaji wa akaunti za makampuni zinalazimu kampuni husika kuwasilisha benki nakala ya usajili wa kampuni, Katiba yake, leseni ya biashara na hati ya mlipa kodi ya TRA (TIN Registration Certificate) kabla ya kuruhusiwa kufungua akaunti. Swali la kujibiwa na NBC pamoja na Serikali ni je, ilikuwaje Tangold Ltd. iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti ya benki kabla hata haijaandikishwa nchini Mauritius achilia mbali kupata hati ya kutimiza masharti ya Tanzania?

Pili, kampuni ya Tangold Ltd. iliendesha akaunti hiyo bila kuweka au kutoa fedha yoyote ile kati ya tarehe 1 Januari 2003 hadi tarehe 1 Agosti 2005 ilipoanza kunyeshewa mvua ya neema ya mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania kutoka BOT! Mvua hiyo ni nje ya mvua ya dola za Marekani 13,340,168.37 zilizohojiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na iliinyeshea Tangold Ltd. kama ifuatavyo:

  1. Tarehe 1 Agosti 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 4,703,221,229.08 kwenda kwenye akaunti ya Tangold Ltd. Tarehe hii ni muhimu sana kwani ndiyo siku ambayo BOT ilifanya pia malipo ya kwanza kwa Deep Green Finance kama ilivyoelezewa katika Taarifa hii;

  2. Tarehe 2 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 244,428,386.15 kutoka akaunti yake hiyo kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Kama tuliyoelezea katika Taarifa hii, tarehe 1 Septemba 2005 Deep Green Finance ililipwa pia shilingi 2,083,255,881.60 na BOT;

  3. Tarehe 8 Oktoba 2005 shilingi za Tanzania 39,761,397.98 zilihamishiwa kwenye akaunti ya Tangold Ltd. kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

  4. Tarehe 12 Oktoba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 1,690,500,000.00 kwenda Meremeta Limited;

  5. Tarehe 23 Novemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 555,300,048.00 kwenda Meremeta Ltd.;

  6. Tarehe 10 Desemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 100,940,489.71 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

  7. Tarehe 12 Desemba 2005, siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 551,060,000.00 kwenda kwenye akaunti ya Meremeta Ltd.

Baada ya hapo Tangold Ltd. haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi tarehe 6 Juni 2006 ilipohamisha shilingi za Tanzania 220,980,370.00 kwenda ‘TISS.’ TISS ni kifupi cha Tanzania Intelligence and Security Service ambalo ni jina la Kiingereza la Idara ya Usalama wa Taifa! Tangu tarehe hiyo hadi leo hii Tangold Ltd. haijaweka wala kutoa fedha nyingine yoyote katika akaunti hiyo. Kwa maana hiyo, katika kipindi cha miezi minne Tangold Ltd. iliingiziwa na BOT jumla ya shilingi za Tanzania 4,742,982,627.06 na ilifanya malipo kwa Deep Green Finance na Meremeta Ltd. ya jumla ya shilingi za Tanzania 3,363,531,259.67.

rudi...     inaendelea...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl