lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Taarifa kwa Umma


VI.  HITIMISHO

Katika tamko lake serikali imetumia uwepo wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kama kigezo cha msingi cha kujenga hoja kwa umma kama serikali inadhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi; wakati serikali ikijivunia kwa ilani hiyo wananchi waendelea kuhushudia vitendo vya rushwa ndani ya CCM yenyewe inayopaswa kusimamia ilani hiyo.

Tunasikitika kwamba serikali imerudia tena kauli yake kwamba wote wanaoibua tuhuma za ufisadi walenga kupandikiza chuki dhidi ya serikali; tunaamini umma wa Watanzania utaamua- ni nani anayepandikiza chuki kati ya anayeficha ama kutetea ufisadi na na sisi tunaotumia haki zetu za kikatiba kujua hatma ya rasilimali na mali zetu?. Hii ni ishara ya kiburi cha serikali iliyolewa madaraka kudhani kwamba serikali ndiyo inayomiliki rasilimali za taifa. Tunaitaka serikali ikumbuke kwamba imechukua dhamana (hold in trust) kwa niaba ya wananchi hivyo ina wajibu wa kujibu inapoulizwa na wanananchi.

Tunapenda kusisitiza kuwa hatutegemei kuwasilisha taarifa yeyote kwa vyombo vya dola kama serikali ilivyoelekeza. Vyombo hivyo vinawataalam, wanalipwa kwa kazi hiyo, walitakiwa kuwa wamefanya upelelezi huo muda mrefu uliopita, taarifa nyingine zimesambaa zaidi ya mwaka sasa. Hakuna hatua iliyochukuliwa wala na Serikali wala na vyombo hivyo. Taarifa tulizozitoa bungeni, kupitia vyombo vya habari na kwa umma wa watanzania mpaka sasa zinajitosheleza kwa vyombo vya dola kuchukua hatua, na sehemu kubwa ya ushahidi tayari uko kwa vyombo hivyo kwa sababu unatoka katika vyombo vya serikali yenyewe. Swali la kujiuliza, wananchi wanapaswa kujiuliza, ni kwanini vyombo vya dola havichukui hatua? Je Dkt. Slaa na viongozi wengine wa upinzani wameitwa kuhojiwa na mahakama au vyombo vingine vya uchunguzi kuhusu tuhuma hizi wakakataa kutoa ushirikiano? Ilishatangazwa hadharani kuwa Taarifa na vielelezo vya Dkt. Slaa vimefikishwa kwa Polisi na ikasemekana kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Serikali ziko ngapi, haiwasiliani na vyombo vyake?

Tunapenda pia kuikumbusha serikali kuwa hoja ya Dkt. Slaa ilifanyiwa mizengwe izuiwe isiingie Bungeni kwa vile ikiingia Bungeni ina athari mbaya kwa Serikali (kwa mujibu wa taarifa ya usalama wa taifa na mtiririko wa matukio). Na kwamba idara ya usalama wa Taifa inachunguza uvujaji wa taarifa (leakage) ambao umefanya nyaraka mbalimbali ziwafikie wapinzani; kama Serikali inatumia fedha za walipa kodi kuchunguza uvujaji wa taarifa (leakage) badala ya kuchunguza ufisadi na ubadhirifu kuna sababu gani ya kupeleka taarifa kwa vyombo hivyo?

Tumeshangazwa na ufafanuzi wa serikali kwamba tuhuma hizi za ufisadi zimetolewa na upinzani kwa sababu ya kushindwa uchaguzi mkuu 2005. Hizi ni fikra za viongozi wasioelewa ama wasiokubali dhana na dhima ya vyama vya upinzani katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Serikali ijieleze kwa wananchi ieleweke isitafute mchawi. Leo wananchi wanalalamika kila kona ya nchi kwamba maisha bora hayajaonekana; wananchi wanalalamikia serikali kutokokutekeleza ahadi zake, vijana wanauliza ajira ziko wapi?, wanawake wanauliza lini watawezeshwa?. Wananchi wanahoji mbona bajeti imewaletea ugumu zaidi wa maisha kutokana na ongezeko la kodi? Watanzania wanauliza kwa nini fedha za kodi zao na michango ya wahisani inapotea kutokana na ubadhirifu na ufisadi? Raia wanauliza mbona faida ya kuwa na maliasili na rasilimali nyingi ikiwemo madini haizonekani katika maisha yao ya kila siku?. Serikali inapaswa kuwajibika kwa wananchi kuhusu masuala haya.

Serikali ikishindwa kujibu hoja hizi tutaendelea kuwakumbusha wananchi kauli yetu tuliyoitoa mwaka 2005 kwamba:

“Mabadiliko ya kweli, hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale, na kulindana vile vile, eti kwa ari, nguvu na kasi mpya; kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema (CCM), Tanzania yenye neema kamwe haiwezekani!"

 

rudi...    

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl