lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Taarifa kwa Umma


II.  TUHUMA KUHUSU WATUMISHI WA UMMA KUSHIRIKI KATIKA KAMPUNI BINAFSI

Tunashukuru kwa serikali kuthibitisha tena kuwa TANGOLD ni kampuni ya Serikali na inamilikiwa na Serikali asilimia mia 100%. Iwapo hii ni kweli:-

  1. Serikali haijaeleza kwanini Kampuni hii ya Serikali ya Tanzania ilisajiliwa Mauritius na kupata tu hati ya kutimiza masharti (Certificate of Compliance) nchini Tanzania tena baadaye? Ilifanya Biashara gani kule Mauritius wakati Sheria ya Mauritius na hati ya usajili ilikataza isifanye Biashara Marititus?

  2. Serikali iwatangaze wahusika wote, ili jamii ya Watanzania iweze kupekua vitabu vya Sheria kama kuna mgongano wa kimaslahi (“conflict of interest”) popote au la ?

  3. Serikali inaitaja tu na haielezi ya kuwa Tanzania tumenufaika nini na Kampuni hiyo na kwanini taarifa ya Tangold haiko kwenye Taarifa ya Ukaguzi, angalau kutaja tu kuwa Benki kuu inahisa katika Kampuni hiyo?

Kwa mantiki hiyo: Haya Maswali yasipopata majibu ya kuridhisha Serikali bado itakuwa imetoa majibu ya kubabaisha. Tunaitaka serikali itoe kwa umma majibu ya maswali hayo.

III.  TUHUMA KUHUSU KAMPUNI YA ALEX STEWART (ASSAYERS):

  1. a) Serikali imekwepa kueleza undani wa suala hili kwa kisingizio kuwa suala hili liko mahakamani. Hata hivyo serikali haijaeleza kesi iliyofunguliwa mahakamani inahusu nini yaani misingi ya ya kesi (grounds of the case) . Ni vema serikali ikasoma hoja husika na /au akaomba faili la kesi husika mahakamani ili aweze kuona grounds zilizoko mahakamani na uhusiano ukoje.

  2. Hoja ya Dkt. Slaa iko wazi kuwa, kuna taarifa zinazotatanisha ya kuwa “Waziri anatuhumiwa kuwa anamiliki asilimia 12.5 ya Hisa ya Kampuni ya Alex Stewart”. Serikali ingelituambia kuwa ilifanya utatifi lini juu ya hilo na walipata majibu gani na ni hatua gani zimechukuliwa na serikali.

Kwa hali hiyo basi: Tunaitaka serikali itoe hadharani mkataba kati ya Benki Kuu (kwa niaba ya serikali) ili kubaini kama kuna hujuma/ufisadi au la, kujitetea kwa maneno matupu hakutoshi. Kinachotakiwa ni majibu ya Serikali siyo kujificha nyuma ya ‘tamko la serikali’.

IV.  TUHUMA KUHUSU MADINI

Suala hili serikali imelitolea ufafanuzi katika tamko tofauti hivi karibuni na kuchapa matangazo katika vyombo vya habari mbalimbali. Bahati nzuri wakati tamko hili linatoka tayari Mkataba wa Buzwagi umeweka hadharani na unaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali. Mkataba ambao ni ushahidi wa wazi wa jinsi ambavyo, kinyume kabisa na Waziri wa Nishati na Madini - Nazir Karamagi alivyosema bungeni, watanzania tutaendelea kutonufaika ipasavyo kutokana na rasilimali za nchi yetu. Katika hatua ya sasa tungependa kuacha umma wa watanzania uendelee kuujadili mkataba huu katika maeneo yao.

Kwa muktadha huo: CHADEMA tutatoa tamko kamili kuchambua kile ambacho serikali imekiita “Maendeleo katika sekta ya Madini”.

V.  TUHUMA ZA RUSHWA KATIKA UNUNUZI NA UBINAFSISHAJI:

  1. Tuhuma tulizotoa katika eneo hili ni mahususi. Tulitaja majina na sababu ya kuwataja. Serikali imejibu juu juu na kuwapotosha watanzania. Kipindi cha majibu ya mafumbo kimeisha, nadhani Serikali hii bado haijagundua hili. Tunahitaji majibu kamili kwa kila tuhuma kama tulivyozitoa. Vinginevyo Watanzania wataendelea kuunika ufisadi huo na kuendelea kuwajadili mafisadi wote waliohusika.
  2. Tumeeleza kwa mfano kwamba zipo taarifa za kuaminika kuwa Plot no 15 Luthuli Street ilitumika kama Ofisi ya Biashara badala ya kuwa Ofisi ya Ikulu, inayolipiwa Kodi na watanzania wote. Kama ni kweli Ofisi yetu ya Plot na 15 Luthuli Street imetumika kama ofisi ya biashara kwa kipindi hicho chote Serikali imekusanya kodi ya pango kiasi gani?

Tunasisitiza kuwa: Maswali yote yaliyohusiana na tuhuma hizo yanahitaji kujibiwa kikamilifu. Serikali haijajibu, na imepoteza fedha za watanzania bure kuchapa matangazo, kuyatawanya na kadhalika jambo ambalo linaongezea matumizi mabaya ya fedha za umma. Tunategemea hali hii haitajirudia tena na badala yake fedha za walipa kodi zitatumiwa vizuri na serikali katika kutoa ufafanuzi wa kutosha na wa kweli kwa umma wa watanzania.

rudi...     inaendelea...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl