Tamko la Vijana wa CHADEMA lililoazimiwa Oktoba 21,2006 na kusambazwa Novemba 14,2006 lilitamka pamoja na mambo mengine nanukuu, "Vijana wa CHADEMA tunatoa mwito kwa vijana wote ambao kwa namna mmoja au nyingine walitapeliwa na serikali kuwasilisha malalamiko yao CHADEMA kwa ajili ya kuanza ufuatiliaji“.
Kadhalika imeandikwa kwenye gazeti la Mwananchi Novemba 23,2006 kwamba "CHADEMA kimewataka wanafunzi walioandikishwa na serikali ili wapewe mikopo ya kujiunga na elimu ya juu na baadaye kurejeshwa nyumbani kwa kunyimwa mikopo hiyo, wafike katika ofisi za chama hicho ili kiwasaidie kupata haki yao".
Tunapenda kutoa ufafanuzi na maelekezo yafuatayo:
Yapo makundi mawili makubwa ya walalamikaji:
Kwa mantiki hiyo wanafunzi waliokosa mikopo kutokana na uamuzi huo wa serikali waliombwa na tunatumia fursa hii kuwaomba tena kuwasilisha malalamiko yao makao makuu ya chama katika kurugenzi ya vijana, wanaweza kuwasilisha malalamiko kwa gharama zao kwa kati ya njia zifuatazo:
- Kwa kufika ofisini (Kinondoni Manyanya, Mtaa wa Ufipa)
- Kwa njia ya simu (022-2668866, 0754-694553, 0754-471751)
- Anauni pepe (vijana@chadema.net)
- Tovuti (www.chadema.net)
- Ama kutuma barua kwa posta (S.L.P 31191, Dar es salaam)
Aidha tunachukua fursa hii kuwapongeza wanavyuo ambao wameitikia mwito huu mpaka sasa, tukumbuke wosia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwamba haki hailetwi kwenye kisahani, inatafutwa.
CHADEMA: Mabadiliko ya Kweli!, Uhuru wa Kweli!
Imetolewa: 23/11/2006
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana