lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

UTANGULIZI

Lifuatalo ni tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu siku 100 za utawala wa serekali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais wa Awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Tamko hili linaeleza mafanikio, mapungufu na kutoa mwelekeo pamoja na mapendekezo.

Tamko hili halihusishi tathmini ya CHADEMA kuhusu Uchaguzi Mkuu 2005, masuala ya uchaguzi uliopita, Mpango kazi wa chama 2006 pamoja na Mkakati wa CHADEMA wa mwaka 2006-2010 yatatolewa tamko baada ya kikao cha Baraza Kuu la chama kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi April. Sehemu kubwa ya masuala haya yalishajadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya CHADEMA kilichofanyika katikati ya mwezi Machi. Hii ni kuruhusu miundo ya chama ikiwemo vikao vya kikatiba kuweza kutekeleza majukumu yake ya kiutawala na kidemokrasia kama ulivyo utamaduni wa CHADEMA.

Pia tamko hili halitagusia ahadi ambazo CCM imezitoa wakati wa kampeni ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa nyingi na za ujumla ambazo nyingi hazikulengwa kutekelezwa ndani ya siku 100. Tamko hili linajikita katika ahadi za serikali na mwelekeo wa kiutendaji mara baada ya kuingia madarakani mpaka baada ya siku 100 za utawala.

Aidha CHADEMA imekuwa kimya kutoa matamko ya mara kwa mara kuhusu utendaji wa serekali toka utawala mpya ulipoingia madarakani ili kutoa fursa kwa serekali kutulia, kupata wasaa wa kutoa mwelekeo na kuanza kutekeleza ahadi zake za msingi.

  Mafanikio...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl