lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Kwa upande mwingine , CHADEMA tunapenda kuionya serikali dhidi ya kauli za kutatanisha ambazo imekuwa ikizitoa kuhusu mustakabali wa siasa na harakati nyingine zenye lengo la kujenga maendeleo kwa madai kuwa ni kupiga siasa huku chama tawala ndio kimekuwa mstari wa mbele katika kupiga propaganda na uzushi kama ambavyo amekuwa akifanya Luten Yusuph Makamba.

Hivi karibuni itakumbukwa kuwa Mh waziri Mkuu Edward amekaririwa na vyombo vya habari akiwataka wanasiasa waache kupiga siasa kwa madai kuwa sasa ni muda wa maendeleo.

Kauli hii kimsingi inautata mkubwa na kama waziri Mkuu hataitolea ufafanuzi inaweza kuleta machafuko yasiyo ya lazima. Kwasababu kimsingi sisi CHADEMA kama chama cha siasa hatuwezi kuacha kuipigia kelele serikali kwa kuionyesha njia mbadala kupitia mikutano ya hadhara na vyombo vya habari.

Sasa kama Mh waziri Mkuu hataki serikali yake ikosolewe kwa madai kuwa sasa ni wakati wa maendeleo sisi CHADEMA hatukubaliani na janja hiyo na kama anataka vyama vikae kimya mpaka wakati wa uchaguzi tunamshauri aandae muswaada wakufuta vyama vingi nchini.

Ingawa kwa upande mwingine kama Lowasa anachopinga ni kampeni za porojo zinazofanywa na Makamba hatuna tatizo, na kimsingi kama maana yake ni hiyo tunamwomba aanze kumshughulikia Makamba.

Kwani anachokifanya Makamba sasa ni kampeni ya kuwahadaa watanzania nchi nzima kitendo ambacho kama hakitadhibitiwa kinaweza kudhoofisha maendeleo.

Mwisho CHADEMA tunapenda kusisitiza msimamo wetu kuwa kazi yetu ni kuleta maendeleo kila tunapopata fursa kama tunavyoendelea kufanya katika halmashauri tunazoziongoza za Karatu na Kigoma Ujiji.

Erasto Tumbo
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

rudi...  

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl