lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Matamko mengine
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

MAPUNGUFU:

Uchaguzi wa Bunge la Afrika ya Mashariki 2006 HAUKUWA HURU WALA WA HAKI kutokana na mapungufu yafuatayo ya msingi.

  1. UFISADI NA SHINIKIZO/MAELEKEZO KWA WAPIGA KURA: Kampeni zilitawaliwa na mapungufu mawili makubwa: Mosi, palikuwa na ufisadi katika kampeni hususani katika makundi yaliyogombewa na wagombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) pekee. Katika lugha rahisi ufisadi unaweza kutafsiriwa kama uozo wa kimaadili ambao unajumuisha rushwa ya fedha, matumizi mabaya ya madaraka nakadhalika. Katika kundi hili la wagombea yalisikika malalamiko toka kwa wagombea mbalimbali kwamba wapo waliokuwa wakitumia rushwa ya fedha, wengine wakitumia sababu za kuwa na ndugu zao ama watu wa karibu yao walioko katika utawala na hivyo kampeni kujikita katika siasa za makundi na kambi mbalimbali. Takribani nusu ya wagombea walioshinda wana undugu na watu mbalimbali katika utawala ama baba, kaka, wanandoa nakadhalika. Pia palikuwa na malalamiko ya kuwepo kwa kampeni za kuchafuana hususani kupitia jumbe za simu za mkono.(SMS). Lakini katika hali ya kushangaza na pengine yenye kuleta hisia za kulindana wagombea hao hao walihutubia na kutangaza kwamba mchakato mzima ulikuwa wa kidemokrasia.

    Kwa upande wa kundi C la upinzani hali ilikuwa mbaya zaidi, kwa ujumla wapiga kura ambao pia ni wabunge wa jamhuri ya Muungano wengi wao walipiga kura kwa shinikizo na maelekezo. Usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura wabunge wa CCM walikutana kama kamati ya chama chao(party caucus). Vyanzo vya kuaminika vimedokeza kwamba kupitia kikao hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa Kikao Mheshimiwa Edward Lowasa ambaye pia ni Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwamba imeamuliwa kura zote za wabunge wa CCM apewe mgombea wa UDP Dk. Fortunatus Masha. Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa hoja hii ilizua mjadala huku wachache wakiipinga waziwazi lakini mwisho shinikizo na maelekezo hayo yalibadili upepo wa uchaguzi. Sababu za kufikia uamuzi huu zilizotolewa ni pamoja na hisia kwamba Profesa Baregu angekuwa na msimamo usiyoyumbishwa katika masuala fulani fulani na kwa upande mwingine hofu kwamba kumpa fursa hiyo ingekuwa ni kama kuijenga CHADEMA kisiasa. Kwa ujumla ufisadi na shinikizo vilifanya wengi ya wabunge wapige kura si kwa kuzingatia zaidi uwezo wa wagombea na maslahi ya taifa na hivyo kufanya uchaguzi kutokuwa huru na wa haki hususani katika kundi la vyama vya upinzani.
Utangulizi...     Ukiukwaji wa kanuni...

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl