Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa CHADEMA iwapo atakidhi sifa kama ilivyoainishwa katika katiba: sifa za kuwa mwanachama ni kama ifuatavyo:
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na umri usiopungua miaka 18.
- Awe na akili timamu.
- Awe anakubaliana na sera, katiba, kanuni na maadili ya chama.
- Awe anakubaliana na itikadi na falsafa ya chama.
- Asiwe mwanachama wa chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA.
- Vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 17 ambao wana mapenzi na chama watapewa kadi maalum kutoka katika baraza la vijana.
- Kuwa ndani ya chama kunampa mtu uwezo pia wa kujiunga na mabaraza ya chama (baraza la vijana, wazee na wanawake).
Majukumu, wajibu na haki za wanachama wa CHADEMA.