Vijana, wasichana na wavulana ni sehemu kubwa ya Taifa – zaidi ya nusu ya Watanzania wote.
Vijana bado wanaonekana ni Taifa la kesho.
Vijana wanatumiwa kama washabiki katika siasa - ushiriki wao katika uongozi ni finyu.
Ukosefu wa ajira kwa vijana unazidi kuongezeka – Hasa vijana wa kike hawana ajira na kujikuta wanajiingiza katika vitendo vya biashara ya ngono.
Vijana wenye vipaji wametelekezwa – vipaji vya vijana haviendelezwi.
Vijana wengi ni hohehahe – vijana wako duni zaidi kiuchumi.
Vijana wanabugudhiwa – wanakamatwa kwa uzururaji, wafanyabiashara ndogondogo wanatimuliwa!
Vijana wanateketea kwa UKIMWI na madawa ya kulevya.
Michezo imepuuzwa na vijana hawana cha kufanya hivo kujiingiza katika uhalifu.
Serikali ya CHADEMA na sura mpya ya Vijana wa Tanzania
Tunaamini kwa vitendo kuwa kijana ni Taifa la Leo.
Tutatoa fursa na kuwezesha kizazi kipya kuwa mstari wa mbele katika siasa, uchumi na sekta nyingine.
Tutaweka mazingira ya kuundwa kwa Baraza Huru la Vijana Tanzania.
Tutawezesha vijana wa kike na wa kiume kumiliki ardhi na rasilimali nyingine kwa kutenga maeneo kadhaa ya biashara kwa vijana tu.
Tutaweka kipaumbele katika kukuza ajira kwa vijana kupitia vipaji vyao katika nyanja mbalimbali – tutazielekeza halmashauri kuanzisha mifuko ya ukuzaji vipaji vya Vijana.
Tutaweka mazingira ya kuboreshwa kwa malezi ya Vijana katika familia na mashuleni ili kukabiliana na UKIMWI na madawa ya kulevya.
Tutatoa leseni za bure na likizo ya kodi kwa Vijana wafanyabiashara ndogondogo na Vijana wanayojishughulisha na uzalishaji mali.
Muziki wa kizazi kipya utapewa kipaumbele ili soko la muziki huu litakuzwa nje ya Tanzania.