lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Seza Zingine
Sera ya Afya
Sera ya Ajira
Sera ya Ardhi
Sera ya Biashara
Sera ya Demokrasia
Sera ya Elimu
Sera ya Kilimo
Sera ya Madini
Sera ya Maji
Sera ya Mazingira
Sera ya Michezo
Sera ya Mifugo
Sera ya Miundombinu
Sera ya Rasilimali
Sera ya Uchumi
Sera ya Ulinzi
Sera ya Utamaduni
Sera ya Utawala
Sera ya Utawala Bora
Sera ya Vijana
Sera ya Viwanda
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part

Sera ya Utawala

lf.bevel rt.bevel
Sera ya Majimbo
Soma mchanganuo makini wa Sera ya Utawala ya Majimbo ulioawasilishwa na Mhe. Masinde
lf.bevel rt.bevel

Utawala wa Ukiritimba na Urasimu, ukoje?

  1. Serikali kuu inaingilia mamlaka ya Serikali za mitaa. Katiba haipo wazi juu ya mamlaka ya serikali za mitaa.
  2. Serikali ni kubwa mno na haina ufanisi.
  3. Halmashauri za Wilaya zimebanwa, hazina uhuru wa kutosha na zinaingiliwa na watawala kutoka Serikali kuu.
  4. Wakuu wa wilaya wanaingilia utendaji wa halmashauri za wilaya na kudhoofisha demokrasia.
  5. Mikoa ni mingi sana na haina ufanisi kiutawala na kiuchumi.
  6. Mfumo wa Muungano ni tata na hautoi nafasi kwa Muungano mkubwa zaidi wa shirikisho la Afrika Mashariki.

Serikali ya CHADEMA itaondoa ukiritimba na urasimu kwa kufanya yafuatayo.

  1. Cheo cha Mkuu wa Wilaya kitafutwa na kazi zote za Ofisi ya Mkuu wa Wilaya zitajuimshwa na Kazi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji pamoja na Meya.
  2. Halmashauri za Wilaya zitapewa mamlaka na uhuru zaidi kwa mujibu wa Katiba Mpya itakayotungwa kwa ushiriki wa wananchi.
  3. Mfumo wa serikali za mitaa utaimarishwa kwa kuimarisha serikali ya Kijiji kama chombo cha msingi cha uongozi (governance).
  4. Mameya watachaguliwa na wananchi moja kwa moja na watakuwa na majukumu ya utendaji pia.
  5. Mikoa ya sasa itaunganishwa na kuwa na mikoa kumi tu ili kuwezesha ufanisi wa kazi na pia kuleta ushindani wa kiuchumi miongoni mwa mikoa ndani ya nchi.
  6. Mikoa itakayoundwa itakuwa na mabunge yao na kuchagua viongozi wao kidemokrasia.
  7. Tutarekebisha mfumo wa Muungano ili kuiweka nchi tayari kwa shirikisho la Afrika Mashariki bila kuathiri uhuru na dola ya Zanzibar na Tanganyika.
  8. Mabadiliko yote ya mfumo wa Utawala wa nchi yatafanywa kufuatia zoezi la kutunga katiba mpya nchi kufuatia
  9. Mkutano Mkubwa wa Katiba utakaoshirikisha wananchi wote.
  10. Nafasi za uongozi wa serikali zitakuwa na mtazamo mkubwa wa kijinsia.
  11. Serikali itakayoongozwa na CHADEMA itahakikisha nafasi za Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu zinashikiliwa na idadi ya kutosha ya Wanawake ili kuweka uwiano wa kijinsia katika utawala wa nchi.
  12. Serikali ya CHADEMA itahakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi katika Mahakama na
  13. Bunge kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake wengi zaidi kusomea sheria na kuajiriwa kuwa mahakimu wa mwanzo, wa wilaya na mahakimu wakazi na baadae kuwa Majaji.
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl