lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Seza Zingine
Sera ya Afya
Sera ya Ajira
Sera ya Ardhi
Sera ya Biashara
Sera ya Demokrasia
Sera ya Elimu
Sera ya Kilimo
Sera ya Madini
Sera ya Maji
Sera ya Mazingira
Sera ya Michezo
Sera ya Mifugo
Sera ya Miundombinu
Sera ya Rasilimali
Sera ya Uchumi
Sera ya Ulinzi
Sera ya Utamaduni
Sera ya Utawala
Sera ya Utawala Bora
Sera ya Vijana
Sera ya Viwanda
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part

Sera ya Rasilimali

Tanzania ni moja kati ya nchi zilizojaliwa utajiri wa maliasili. Ni nchi yenye mito, mabonde, maziwa, vito vya thamani, wanyamapori, milima, misitu na vingine vingi ambavyo kama vitatumika vizuri vinaweza kuliletea taifa letu maendeleo ya haraka katika sekta karibu zote.

Lengo kuu la sera hii ni kurudisha rasilimali za nchi mikononi mwa wananchi wenyewe ili wawe na wajibu na haki katika matumizi, ugawaji na utunzaji wa rasilimali zilizopo kwa manufaa ya Taifa letu.

Kimsingi sera hii ya maliasili inalenga sekta kuu sita:

1.   Sekta ya Wanyapori

  1. Kuhimizwa kwa wananchi wenye nia na uwezo wa kuwekeza katika maeneo yafuatayo: Ufugaji wanyamapori; Kuendesha shughuli za safari za uwindaji; Kuendesha shughuli za upigaji wa picha za wanyamapori kitalii; and Kujihusisha na biashara ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori.

  2. Kuwapa kipaumbele wazalendo katika kujifunza na kufanya utafiti wa wanyamapori.

  3. Itakuwa ni marufuku kwa wageni kusafirisha au kuhamisha wanyama walio hai, badala yake kazi hiyo itafanywa na wananchi wenyewe.

2.   Sekta ya Uvuvi

  1. Kuwawezesha wawekezaji wazalendo kupata teknolojia ya kisasa ili kuongeza pato la Taifa kwa kuongeza kiasi cha mazao ya uvuvi.

  2. Kuweka mkakati utakaowawezesha wavuvi wadogowadogo kuwa na uhakika wa soko la mazao yao. Aidha Kuweka sheria itakayowalazimu wavuvi wakubwa hasa wenye viwanda vya usindikaji kununua toka kwa wavuvi wadogo wadogo.

3.   Sekta ya Ufugaji wa Nyuki

  1. Lengo la sera hii ni kufanya ufugaji wa nyuki kuendeshwa kibiashara zaidi, na hii inatokana na kwamba mazao yatokanayo na nyuki bado hayajapatiwa soko la uhakika ukizingatia kwamba aina ya nyuki wanaopatikana katika nchi yetu ndiyo wanaoongoza kwa utoaji wa asali nzuri katika soko la dunia.

  2. Kutolewa kwa elimu muafaka juu ya ufugaji mzuri wa nyuki kibiashara.

  3. Kuongeza juhudi za kutafuta soko la nje na kuchukua jitihada za makusudi katika kuitangaza asali yetu.

4.   Sekta ya Misitu

  1. Kufuta utaratibu holela wa uvunaji wa misitu iliyopo hivi sasa.

  2. Kuweka upendeleo kwa wananchi kuvuna na kuuza mazao ya misitu.

  3. Kuhimiza uwepo wa misitu ya kupandwa.

5.   Sekta ya Nishati

    Kufanywa kwa utafiti wa kina zaidi juu ya matumizi ya kuni vijijini ili kupata nishati mbadala na isiyo aghali, ili kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na kukatwa kwa miti.

  1. Kuwekeza katika utafutaji wa mafuta katika mwambao wa nchi yetu na kuendesha uchimbaji wake iwapo itathibitika kwamba uchimbaji wake unaweza kufanyika kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake.

  2. Kuchukuliwa kwa hatua za makusudi ili kupunguza bei ya umeme. Na hili litawezekana iwapo tutakuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika.

  3. Sehemu za vijijini ambako umeme haujafika, CHADEMA kitaweka utaratibu maalum wa kusambaza vifaa vya kutumia nishati ya jua kwa gharama nafuu ili wananchi waweze kulitumia kama nishati mbadala.

6.   Sekta ya Utalii

  1. Kuchukua hatua za makusudi ili kuimarisha miundombinu yote inayoelekea sehemu za kitalii.

  2. Kuhakikisha kwamba moja kati ya kazi za balozi zetu ni kutangaza vivutio vyetu vya utalii.

  3. Kuboresha na kuimarisha vituo vya utalii wa mambo ya kale, ili kuinua mapato yanayotokana na eneo hilo.

  4. Wananchi waishio katika maeneo yazungukayo sehemu za kitalii washirikishwe katika mipango yote ihusuyo maeneo hayo. Aidha mipaka ya sehemu zilizotengwa kwa ajili ya utalii ni lazima ikubalike na wananchi hao.
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl