lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Seza Zingine
Sera ya Afya
Sera ya Ajira
Sera ya Ardhi
Sera ya Biashara
Sera ya Demokrasia
Sera ya Elimu
Sera ya Kilimo
Sera ya Madini
Sera ya Maji
Sera ya Mazingira
Sera ya Michezo
Sera ya Mifugo
Sera ya Miundombinu
Sera ya Rasilimali
Sera ya Uchumi
Sera ya Ulinzi
Sera ya Utamaduni
Sera ya Utawala
Sera ya Utawala Bora
Sera ya Vijana
Sera ya Viwanda
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part

Sera ya Miundombinu

Nchi yetu ina maeneo mbalimbali yenye bidhaa, neema na utajiri wa rasilimali tele zinazohitajika sana maeneo mengine. Karibu kila kitu kinapatikana hapa hapa nchini kwa ajili ya maisha yetu na ya wengine.

Lakini kutokana na kukosekana kwa miundombinu, maeneo mengi nchini yanakosa bidhaa kutoka maeneo mengine, na kisha kuathiri ukuaji wa soko la ndani na kuwafanya wananchi wakose mahitaji muhimu. Tunashuhudia watu wakiwa na njaa maeneo fulani ya nchi huku wengine wakiharibikiwa na mazao. Katika hali hii, uchumi wa nchi umekuwa ukidorora kwasababu ya kukosa miundombinu ya uhakika na kusababisha watu wengi kushindwa kuendelea.

  1. Miundombinu inayotakiwa kujengwa, kuimarishwa na kupanuliwa katika nchi kavu ni barabara, reli na mabomba. Hivyo basi, wahandisi na makandarasi wa barabara na reli, watapewa zabuni za ujenzi kwa usimamizi wa vyombo vya kuchaguliwa na wananchi, yaani Bunge na halmashauri. Pia washindi wa zabuni watapitishwa na Bunge na Halmashauri kwa uwazi.

  2. Hivi sasa upo mpango wa kujenga barabara kuu muhimu katika kiwango cha lami ambao utagharimiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAM). CHADEMA haitasubiri mpaka nchi tatu ziafikiane, ila itahakikisha kwamba barabara zote kuu zinaounganisha mikoa na kanda zinajengwa katika kiwango cha lami.

  3. Sheria ya Usalama barabarani (Road Traffic Act 1973) itakuwa chini ya Wizara mpya ya Miundombinu badala ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Usalama wa barabara na magari utatofautishwa na usalama wa raia. Wahandisi wa magari na barabara ndiyo watahusika na ukaguzi wa magari na barabara badala ya askari polisi.

  4. Kwenye miji mikubwa, na hususan Dar es Salaam, ujenzi wa barabara zinazopita juu (flying roads) utaanzishwa maramoja ili kupunguza msongamano wa magari na uchelewaji kazini.

  5. Matumizi na ujengaji wa reli utaendelezwa pamoja na kurudishia reli iliyong’olewa ya Mtwara hadi Nachingwea. Njia nyingine mpya za reli zitatafitiwa, kupimwa na kujengwa. Maeneo ambayo yanafaa kujengwa reli haraka ni Mtwara hadi Songea kupitia Nachingwea na Tunduru; Makambako hadi Mbambabay kupitia Mbinga; Arusha hadi Musoma kupitia Serengeti; na Tunduma hadi Mpanda kupitia Sumbawanga.

    Pia CHADEMA itaweka utaratibu wa kupanua reli ya kati kutoka Shinyanga hadi Bukoba kupitia Nyakanazi na Biharamulo; na Dodoma hadi Tanga kupitia Kondoa, Kiteto na Handeni. Maeneo mengine yanayohitaji reli ni Singida hadi Arusha kupitia Katesh; Tabora hadi Mbeya kupitia Chunya; Iringa hadi Singida kupitia Manyoni; Ifakara hadi Tunduru kupitia Mahenge na Liwale; na Dar es Salaam hadi Mtwara kupitia Lindi.

  6. CHADEMA itaanzisha utaratibu wa kusafirisha mafuta kutokea Dar es Salaam au sehemu zenye mafuta kwenda mikoa iliyo mbali kama Kagera, Mwanza, Arusha, Musoma, Ruvuma, Tabora, Manyara, Rukwa, Singida na Kigoma kwa kutumia mabomba ya mafuta ili kuondoa gharama za kutumia usafiri aghali wa barabara au reli na hivyo kupunguza bei ya mafuta mikoani.

  7. Serikali ya CHADEMA itaweka jitihada za makusudi kwa wafanyabiashara wazawa zitakazowawezesha au kuwapa nguvu za kuimudu biashara ya uchukuzi na usafirishaji majini.

    Uwezo wa wazawa kuendesha bandari umejionyesha katika kitengo cha upakiaji na upakuaji katika bandari ya Dar es Salaam ambacho kilikuwa kinaleta faida ya shilingi bilioni 10 kwa mwaka tofauti na sasa ambapo kimeshuka hadi kufikia bilioni 0.4 baada ya kubinafsishwa na wageni.

  8. Sera ya CHADEMA itakazania katika ujenzi wa viwanja vya ndege utakaoendana na kutangaza utalii na vivutio vya kitaifa. Serikali ya CHADEMA pia itanunua ndege kwa ajili ya kuwakodishia au kuwakopesha wafanyabiashara wazalendo ili kuwapa uwezo wa uendeshaji na ushindani katika usafiri wa uchukuzi wa anga.

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl