|
|
|
|
|
|
Sera ya Michezo
Hali ikoje?
- Kuna ukosefu wa viwanja vya michezo - Viwanja vya michezo vimetelekezwa na viko katika hali mbaya.
- Viwango vya michezo ni duni na wenye vipaji hawaendelezwi.
- Tanzania tumepotea katika ramani michezo duniani - Hakuna mchezo wowote kama nchi tunaojivunia kufanya vizuri.
- Michezo mingi imeachwa chini ya viongozi matapeli – wananchi wamebakia kuwa washabiki.
- Mashindano ya mashule yamefutwa na michezo imeondolewa katika ratiba za kawaida za shule.
Serikali ya CHADEMA itafanyaje?
- Tutaziagiza halmashauri kuweka mazingira ya kujengwa vituo vya michezo vyenye viwanja katika kila wilaya.
- Tuboresha muundo wa Baraza la Michezo (BMT) nchini ili kuwa na uwakilishi mpaka katika ngazi ya wilaya.
- Tutarejesha viwanja vilivyotaifishwa na kuviweka chini uangalizi wa BMT kwa kusudio la kuweza kuviendeleza.
- Vilabu vya mpira wa mguu vitatakiwa kuendeshwa kibiashara.
- Itahamasisha uwekezaji katika vituo vya vijana (yoso) wenye vipaji, hususan kandanda na riadha ili kuwaendeleza mpaka kufikia kiwango cha kuliwakilisha taifa letu kimaatifa.
- Tutarejesha na kuhimiza michezo katika mashule na vyuo – michezo itaingizwa katika ratiba na mitaala, mashindano ya shule na vyuo yatarejeshwa na kupewa mkazo.
- Itaanzisha siku ya michezo nchini itakayofanyika kitaifa na katika ngazi ya wilaya.
|
|
 |
 |
|
 |
 |
|