|
|
|
|
|
|
Sera ya Mazingira
Hali ikoje kwa mazingira yetu?
- Mazingira ya mijini ni machafu sana – huduma za uzoaji taka na usafishaji miji ni hafifu, miundombinu ya maji taka haifai.
- Jangwa lazidi kujongea na mvua sio za uhakika tena.
- Wawekezaji hususan wa maeneo ya madini na viwanda, wanaharibu mazingira.
Serikali ya CHADEMA itafanya nini kuboresha mazingira?
- Itaanzisha mashindano ya usafi wa mazingira na bustani za mapumziko kwa halmashauri za wilaya.
- Itahamasisha kila Mtanzania apande na kulea mti mmoja kila mwaka.
- Sheria zatatungwa kulazimisha wawekezaji kutunza mazingira hususan, maeneo ya machimbo ya madini
- Utunzaji wa mazingira itakuwa ni jukumu la serikali za Mitaa na serikali kuu itashughulikia sera na kusimamia utekelezaji wa sera tu.
|
|
 |
 |
|
 |
 |
|