|
|
|
|
|
|
Sera ya Madini
Hali ikoje katika utajiri wetu wa madini?
- Tanzania imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali.
- Katika kila shilingi mia inayopatikana kwenye madini Tanzania inapata shilingi tatu tu!
- Mapato yanoyopatikana kutokana na madini bado hayamfikii wala kumnufaisha Mtanzania
- Mikataba ya uchimbaji wa madini imetawaliwa na usiri mkubwa na inanuka rushwa.
- Vijana wa Kitanzania wafanyao kazi kwenye migodi ya wageni ni sawa na manamba na watumwa ndani ya nchi yao.
- Wachimbaji wadogowadogo wanafukuzwa na kunyimwa fursa ya kumiliki migodi.
Serikali ya CHADEMA itafanya nini Tanzania ifaidi utajiri wa Madini?
- Si chini ya asilimia thelathini ya mapato yatokanayo na madini yatabaki nchini.
- Mikataba yote ya uchimbaji itapitiwa upya na kuwekwa wazi kwa wananchi.
- Kuwekwa sheria na utaratibu zitakazowalinda Watanzania wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini hususan wachimbaji wadogowadogo.
- Kugawa maeneo ya uchimbaji kulingana na mahitaji halisi ya wananchi ili kuzuia migogoro iliyopo hivi sasa.
- Kutoa mikopo na ushauri wa kitaalamu kwa wachimbaji wadogo na kujihusisha na utafutaji wa teknolojia ya kisasa ya uchimbaji.
- Wanawake wafanyao biashara za madini watajengewa uwezo zaidi ili kulinda biashara zao dhidi ya utapeli na pia kuwawezesha kujiendeleza zaidi na kupata masoko ya biashara zao.
- Wachimbaji wadogo wadogo wa Kitanzania watawezeshwa kumiliki maeneo ya uchimbaji kama mbinu ya kuzalisha ajira kutokana na sekta ya madini.
- Mamlaka za serikali za Mitaa ambayo migodi ya madini au visima vya mafuta vipo zitashiriki kwa kiasi kikubwa katika kuandaa mikataba ya uchimbaji wa madini na mafuta.
- Mapato yanayotokana na madini yatatumika katika kuwekeza katika elimu kwa vijana wa Kitanzania.
- Usafishaji wa madini angalau kwa hatua za awali ni lazima ufanyike Tanzania ili kutoa ajira na pia kuchangia ukuaji wa uchumi na pato la wananchi.
- Tenda zote za ugavi kwa makampuni ya madini kwa bidhaa zinazoweza kupatikana Tanzania zitatolewa kwa Watanzania tu. Makampuni ya kigeni hayataruhusiwa kufanya ugamvi wa vitu kama vyakula, kwa mfano!
|
|
 |
 |
|
 |
 |
|