|
|
|
|
|
|
Sera ya Kilimo
Kilimo chetu kidemorora, kwa nini?
- Watanzania wengi bado wanalima kwa kutumia jembe la mkono.
- Kilimo bado kinategemea huruma ya mwenyezi Mungu kupata mvua.
- Soko finyu la mazao ya kilimo – Mengi yanaozea shambani, au kuuzwa kwa bei ya kutupa.
- Mifumo mibovu ya kuhifadhi na kusindika mazao ya kilimo.
- Sera potofu za soko holela zimeua kabisa motisha ya wakulima wa mazao ya chakula na yale ya biashara.
- Bado tunategemea mazao ya biashara tuliyorithi kutoka kwa wakoloni.
- Barabara hazifiki vijijini na hivyo mazao ya wakulima kuoza kabla ya kufika sokoni.
Serikali ya CHADEMA itafanya nini kurejesha hadhi ya kilimo na Wakulima?
- Kodi zote za pembejeo za kilimo zitafutwa ikiwemo VAT.
- Itatilia mkazo wa kipekee barabara zingiazo vijijini.
- Tutatumia mabonde yote, mito na maziwa katika kilimo cha umwagiliaji maji.
- Tutarejesha vyama huru vya ushirika na mali zake.
- Serikali itadhibiti ya soko holela ya mazao ya kilimo.
- Tutatoa ruzuku kwa wakulima wetu ili wazalishe chakula cha kutosha na pia kupambana na ushindani wa bidhaa hafifu kutoka nje.
- Tutatoa motisha kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara km maua, viungo, mboga.
- Tutatoa motisha katika sekta ya usindikaji ya mazao ya kilimo – maelekezo kwa halmashauri ya wilaya kuweka mazingira ya uwekezaji katika usindikaji wa mazao yapatikanayo ndani ya wilaya.
- Serikali itashirikiana na nchi zingine zinazoendelea kushinikiza nchi zilizoendelea kulegeza masharti ya kuuza bidha zetu za kilimo katika masoko yao.
- Tutalinda soko la ndani la bidha zetu.
- Tutatafsiri kilimo sio tu kuishia katika kulima na kuvuna bali kwenye kuzindika na kuongeza thamani ya bidhaa.
|
|
 |
 |
|
 |
 |
|