|
|
|
|
|
|
Sera ya Elimu na Elimu ya Uraia
Hali ya Elimu yetu Tanzania ikoje?
- Elimu bado ni ya kikoloni inayozalisha watwana.
- Mitaala haiendani na hali halisi ya kidunia.
- Wanafunzi wanalazimishwa kusoma kila somo kupata vyeti wakati vipaji haviendelezwi.
- Mpango wa Elimu ya Msingi wa kudandia uliyogubikwa na rushwa – Maandalizi ya walimu ni duni na rasilimali hazifikii walengwa.
- Bajeti ya elimu finyu sana – asilimia 9 tu!
- Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mwisho duniani ambayo kiuwiano na idadi yake ya watu, ina idadi ndogo ya wasomi wa sekondari na vyuo.
- Elimu inawezeshwa kwa fedha za mikopo na misaada ya wahisani wakati fedha itokanayo na kodi atozwayo mwananchi inafanyiwa anasa tu.
- Gharama za elimu bado ni mzigo mkubwa kwa familia masikini.
- Mazingira ya elimu ni duni – madarasa, nyumba za walimu, maabara na vitabu.
- Mfumo wa Elimu hauna mtazamo wa Kijinsia hivyo hauweki mazingira mazuri ya kupata maarifa kwa wanafunzi wa kike na pia wanafunzi wenye ulemavu.
- Mazingira ya shule haya kidhi haja na sio rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa viungo,wasioona na viziwi.
- Elimu ya teknohama hususan sayansi ya kompyuta haijaanzishwa.
- Mfumo wa elimu unaochelewesha kuhitimu – kuchelewa kuanza (miaka 7+) na kuchelewa kumaliza (2,7,6,3+)
- Elimu ya Uraia ni finyu na potofu.
- Michezo mashuleni imefutwa na hivyo kuziba vipaji vya watoto mfano UMITASHUMTA na UMISETA.
Serikali ya CHADEMA itafanyaje ili kuboresha Elimu ya Tanzania?
- Itabadili mitaala ya elimu – Italenga mahitaji na maslahi ya Taifa, mitaala itakayochochea fikra, udadisi, ugunduzi na kuendeleza vipaji.
- Itatenga kwa sekta ya Elimu na Elimu ya Uraia asilimia 35% ya bajeti yote ya Serikali – italenga kuboresha mazingira ya elimu, ya ufundishaji na uboreshaji wa maslahi ya Waalimu na kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu kupata elimu bila vikwazo
- Kamwe elimu haitategemea misaada ya wafadhili na hatutakopa ili kusomesha Watanzania. Elimu italipiwa na fedha za ndani kutokana na makusanyo ya mapato ya kodi na pia mkakati utawekwa ili mapato yote yanayotokana na uchimbaji wa madini yalipie elimu ya watoto wa Tanzania.
- Tutajali walimu kwa kuboresha kipato, makazi na mafunzo yao.
- Mfumo wa elimu utarekebishwa kwa kiasi kikubwa na utakuwa na mtazamo wa kijinsia ili tuoe fursa sawa kwa wananfunzi wa kike na wenye ulemavu katika kujifunza.
- Elimu itatolewa bure kutoka CHEKECHEA mpaka SEKONDARI.
- Tutashirikisha wadau wote muhimu kuweka mfumo wa elimu unaowahisha kuhitimu – kuwahi kuanza (miaka 5) na kuwahi kumaliza (2,6,4,3+)
- Elimu ya msingi itakuwa mpaka darasa na tisa (Kidato cha Pili) na itakuwa ni lazima kwa kila mtoto anaeishi Tanzania.
- Ushirikishwaji wa jamii na wanafunzi katika uendeshaji wa shule utaimarika ili kuboresha ufundishaji na uwazi katika matumizi ya pato la shule.
- Elimu sahihi ya Uraia inayochochea kujitambua na uzalendo itafundishwa katika ngazi zote.
- Kila mwanafunzi wa sekondari atafundishwa somo la sayansi ya kompyuta na utumiaji wa kompyuta.
- Tutageuza majengo yote ya Serikali Dodoma kuwa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi kwa kuendelea na azma yetu ya kuachilia mbali mpango wa kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma. Dodoma itakuwa ni jiji la vyuo na kitovu cha elimu cha nchi.
- Uendeshaji wa shule za msingi na sekondari itakuwa ni jukumu la Serikali za Mitaa na Serikali kuu itatunga sera, kusimamia utekelezajiwa sera na kugawa rasilimali kama fedha.
- Tutaelekeza kila halmashauri kwa kutumia rasilimali zao kuanzisha vyuo vya ufundi katika kila wilaya.
- Tutatoa kipaumbele katika elimu ya ujasiriamali ili Watanzania waweze kujiajiri baada ya masomo.
- Tutarejesha masomo ya biashara katika shule za sekondari ili kuwajenga vijana wa Kitanzania waweze kujiajiri.
- Tutao ruzuku kwa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Tutabadili shule za serikali kuwa ni vituo vya ubora wa elimu ili kuondoa matabaka.
|
|
 |
 |
|
 |
 |
|