lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Seza Zingine
Sera ya Afya
Sera ya Ajira
Sera ya Ardhi
Sera ya Biashara
Sera ya Demokrasia
Sera ya Elimu
Sera ya Kilimo
Sera ya Madini
Sera ya Maji
Sera ya Mazingira
Sera ya Michezo
Sera ya Mifugo
Sera ya Miundombinu
Sera ya Rasilimali
Sera ya Uchumi
Sera ya Ulinzi
Sera ya Utamaduni
Sera ya Utawala
Sera ya Utawala Bora
Sera ya Vijana
Sera ya Viwanda
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part

Sera ya Demokrasia

Hali ikoje?

  1. Nchi inaongozwa kiimla.
  2. Mfumo wa vyama vingi umegubikwa na mizengwe.
  3. Chama kimoja kimehodhi kila kitu.
  4. Sheria zinagandamiza uhuru na ukweli.
  5. Upeo mdogo wa wananchi katika masuala ya demokrasia.
  6. Vyombo vya uwakilishi kama Bunge na Baraza la madiwani havina meno.
  7. Mfumo mbaya wa uchaguzi usiothamini kila kura ya mwananchi.

Serikali ya CHADEMA itafanyaje?

  1. Tutashirikisha wananchi wote kuandika Katiba upya.
  2. Tutaongoza kwa misingi ya sheria na haki za binadamu.
  3. Tutatoa fursa ya vyama vya siasa kujiimarisha.
  4. Tutabadili mfumo wa uchaguzi na kuwa na mfumo mchanyato wa uwiano wa kura na tulio nao sasa ili kuongeza usawa wa kijinsia katika Bunge na pia kuimarisha vyama vya siasa kama asasi muhimu katika ujenzi wa nchi. Chini ya mfumo mpya wa uchaguzi wagombea binafsi wataruhusiwa bila bugudha yeyote.
  5. Tutatenganisha bayana wajibu na mamlaka ya mihimili mitatu ya uendeshaji wa nchi – Bunge, Mahakama na Dola. Wabunge hawatakuwa mawaziri.
  6. Tutafuta sheria zinazobana Asasi za Serikali kufanya kazi zake.
  7. Tutaimarisha Asasi zisizo za kiserikali ili zifanye kazi zake kwa ufanisi na kwa uwajibikaji mkubwa.
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl