lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Seza Zingine
Sera ya Afya
Sera ya Ajira
Sera ya Ardhi
Sera ya Biashara
Sera ya Demokrasia
Sera ya Elimu
Sera ya Kilimo
Sera ya Madini
Sera ya Maji
Sera ya Mazingira
Sera ya Michezo
Sera ya Mifugo
Sera ya Miundombinu
Sera ya Rasilimali
Sera ya Uchumi
Sera ya Ulinzi
Sera ya Utamaduni
Sera ya Utawala
Sera ya Utawala Bora
Sera ya Vijana
Sera ya Viwanda
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Sera ya Utawala Bora

Hali ikoje?

  1. Rushwa na upendeleo vimekithiri katika nyanja zote - Rushwa sasa imekuwa utamaduni.
  2. Shughuli za vyama vya siasa zinafanywa na vyombo vya dola.
  3. Matumizi ya anasa ya viongozi ilhali wananchi wamezamishwa kwenye umaskini uliokithiri.
  4. Viongozi kutowajibika mbele ya wananchi.
  5. Wizi wa mali ya umma, ubinafsishaji holela na ufisadi.
  6. Uuzaji wa nyumba za Serikali kwa viongozi kiupendeleo.
  7. Mamlaka ya Umma imeporwa na tabaka la watu wachache.
  8. Ukosefu wa maadili ya Taifa.
  9. Viongozi wabovu wasiokuwa na dira.
  10. Viongozi wanakula njama na wageni kuhujumu rasilimali zetu.
  11. Hakuna morali.
  12. Ubinafsi umetawala.
  13. Uzembe umekithiri.
  14. Viongozi wasiojali nchi na watu wake.
  15. Mwizi ni yule anayekamatwa, asiyekamatwa ruksa.

Serikali ya CHADEMA itafanyaje?

  1. Itafuta PCB na kuunda upya idara ya kupambana na rushwa chini ya idara ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai.
  2. Idara ya Usalama wa Taifa itafanyiwa marekebisho makubwa ili ilinde maslahi ya nchi na sio ya wakubwa wachache.
  3. Tutaita Mkutano wa Katiba ndani ya mwaka mmoja wa utawala wa CHADEMA.
  4. Katiba kuwa na kipengele kitakacho ruhusu wananchi kuwawajibisha madiwani, wabunge na wawakilishi “recalling clause”.
  5. Itapiga marufuku uuzaji wa nyumba za Serikali na kurejesha zilizokwisha uzwa kiupendeleo.
  6. Matumizi yote ya gharama kubwa bila stahili kusimamishwa mara moja.
  7. Tutakomesha rushwa na atakayetoa au kupokea rushwa atahukumiwa adhabu kali.
  8. Upendeleo utapigwa vita.
  9. Viongozi wa CHADEMA watajali nchi na watu wake.
  10. Tutahamasisha maadili ya Taifa.
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl