lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
Seza Zingine
Sera ya Afya
Sera ya Ajira
Sera ya Ardhi
Sera ya Biashara
Sera ya Demokrasia
Sera ya Elimu
Sera ya Kilimo
Sera ya Madini
Sera ya Maji
Sera ya Mazingira
Sera ya Michezo
Sera ya Mifugo
Sera ya Miundombinu
Sera ya Rasilimali
Sera ya Uchumi
Sera ya Ulinzi
Sera ya Utamaduni
Sera ya Utawala
Sera ya Utawala Bora
Sera ya Vijana
Sera ya Viwanda
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Sera ya Biashara

Kwa nini Tanzania inafanya biashara ya uchuuzi?

  1. Mitaji bado ni ndoto kwa wafanyabiashara na hasa wanawake na vijana kutoka familia za kimasikini.
  2. Kutishwa mzigo wa kodi kubwa.
  3. Ushindani usio sawa – Wafanyabiashara wa nje wanakandamiza wa ndani na wafanyabiashara wakubwa wanakandamiza wadogo.
  4. Bidhaa zenye ubora hafifu.
  5. Ukosefu wa soko la nje.
  6. Rushwa na Upendeleo kwa makusudi ya kisiasa.
  7. Wafanyabiashara wachuuzi.
  8. Wafanyabiashara wadogowadogo, Machinga, wananyanyaswa.
  9. Ushiriki hafifu katika mashirika ya kibiashara kama Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  10. Serikali kujitoa COMESA bila kujali maoni ya wafanya biashara wa ndani na matokeo yake kusababisha hasara kubwa kwa nchi.
  11. Mikataba mibovu ya kimataifa bila kushirikisha wananchi.

Serikali ya CHADEMA itafanyaje kuimarisha biashara?

  1. Tutaimarisha upatikanaji wa mitaji .
  2. Tutaondoa kodi zisizo za lazima hususan kwa wafanyabiashara wazawa.
  3. Tutatekeleza sheria ya ushindani sawa wa kibiashara.
  4. Tutaimarisha utendaji wa shirika la viwango la Tanzania ili kuongeza ubora wa bidhaa zetu.
  5. Tutaimarisha na kutoa nguvu zaidi za kifedha kwa shirika la SIDO ili liwezeshe vijana kujiajiri kwa kuanzisha biashara na viwanda vidogo.
  6. Tutaziagiza balozi zetu kuwa vituo vya biashara.
  7. Tutakomesha rushwa za aina zote katika utoaji wa leseni, zabuni na misamaha ya kodi.
  8. Itakuwa mwiko kwa wanasiasa kuingilia shughuli za wafanyabiashara.
  9. Tutarasimisha na kuwezesha Wamachinga kufanya biashara zao kwa uhuru.
  10. Tutaimarisha mashirika kama TCCIA, Chamber of Mines, CTI na mengineyo ili kuwa sauti ya sekta binafsi.
  11. Tanzania itajiunga tena COMESA kwa kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki kama chombo kikuu cha kujadiliana masuala ya kibiashara na mashirika mengine. Lakini Tanzania haitajitoa SADC ili kuimarisha ushirikiano wa kindugu na rafiki zetu nchi za Kusini mwa Afrika.
  12. Tanzania itafanya mashauriano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya (EPA) kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki kama sehemu ya COMESA.
  13. Majadiliano yote ya kibiashara yatawashirikisha wananchi kupitia Asasi Zisizo za Kiserikali na Asasi binafsi kama TANGO, TCCIA na CTI ili kuweka mbele masilahi ya nchi.
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl