lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Seza Zingine
Sera ya Afya
Sera ya Ajira
Sera ya Ardhi
Sera ya Biashara
Sera ya Demokrasia
Sera ya Elimu
Sera ya Kilimo
Sera ya Madini
Sera ya Maji
Sera ya Mazingira
Sera ya Michezo
Sera ya Mifugo
Sera ya Miundombinu
Sera ya Rasilimali
Sera ya Uchumi
Sera ya Ulinzi
Sera ya Utamaduni
Sera ya Utawala
Sera ya Utawala Bora
Sera ya Vijana
Sera ya Viwanda
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Sera ya Afya

Hali ya afya Tanzania ikoje?

  1. Serikali imekwepa jukumu lake la kutoa huduma za afya kwa wananchi, imelifanya kuwa la kibiashara kuliko huduma.
  2. Huduma za afya nchini zimezidi kupororoka siku hadi siku.
  3. Bajeti ya Wizara ya Afya haina mtazamo wa kijinsia kwani madawa mengi yanayoagizwa nchini ni ya magonjwa ya jumla.
  4. Mpango wa afya ya msingi umeshindikana – wananchi wenye uwezo wanatibiwa na wasio na uwezo wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kama malaria na kipindupindu.
  5. Wanawake wajawazito hawana uhakika wa maisha yao wakati wa kujifungua kwani katika kila wanawake elfu moja wanaojifungua sita hupoteza maisha yao kwa sababu ya mfumo mbaya wa afya usiojali kazi muhimu ya kuzaa.
  6. Ni wanawake 47 tu kati ya wanawake mia moja wanajifungulia hospitalini. Mafunzo kwa wakunga wa jadi hayatoshi na hakuna juhudi za kutatua tatizo hili.
  7. Maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya afya ni finyu.
  8. Pesa za vita dhidi ya ukimwi zinaishia mifukoni mwa wajanja wachache.
  9. Upanuzi wa sekta ya afya haulingani na ongezeko la watu – Daktari mmoja anahudumia wagonjwa.
  10. Wagonjwa wachache sana wa Ukimwi wanapata madawa ya kurefusha maisha – madawa mengi yaliyotolewa kwa msaada yanaporwa na vigogo.
  11. Gharama za afya bado ni mzigo mkubwa kwa wananchi wa kawaida kiasi cha kupelekea kujitibu kwa matabibu wasiyofuzu ilhali viongozi wakitibiwa nje kwa kodi ya wananchi.
  12. Mzigo wa kulea wagonjwa wa Ukimwi limeachwa kwa akina mama majumbani peke yao bila msaada wowote wa serikali (serikali kuu na serikali za mitaa).

Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kuboresha huduma za Afya?

  1. Kupanua mpango wa bima ya afya kumshirikisha kila Mtanzania. Mkazo utawekwa katika kusisitiza ‘lishe bora’ na siyo ‘bora lishe’ – miongoni mwa wananchi Mamlaka za serikali za Mitaa zitaunda mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa wananchi ili kuweka bima ya Afya kwa wananchi wengi vijijini.
  2. Mfumo wa Afya utajengwa kuanzia ngazi ya kijiji ili kupata mahitaji halisi ya madawa kutoka na historia ya magonjwa katika maeneo husika.
  3. Tutahakikisha bajeti ya wizara ya afya inakuwa na mtazamo wa kijinsia kwa kujali sana madawa muhimu kwa akina mama kufuatia masuala ya kimaumbile.
  4. Nguo za watoto wachanga kama nepi n.k hazitatozwa kodi VAT.
  5. Madawa yote muhimu kwa akina mama wajawazito na watoto hayatakuwa na kodi ya forodha na pia VAT.
  6. Ushuru wa forodha na VAT kwa vifaa vya hedhi utakuwa sifuri.
  7. Hamasa itatolewa kwenye utafiti, utumiaji na uboreshaji wa tiba zetu za asili.
  8. Elimu ya afya itatolewa ikiwemo kuhusu lishe ili kurekebisha mila na desturi ambazo zinaathiri afya ya jamii.
  9. Huduma zitakazolipiwa na serikali nje ya nchi ni zile tu zisizopatikana nchini na kwamba wananchi wote watapewa haki sawa ya kupata nafasi hizo.
  10. Vituo vya afya vitaanzishwa vijijini kuwapunguzia wananchi umbali wa kutembea kutafuta huduma za msingi.
  11. Itawajali na kuwahudumia Watanzania wenye kuishi na virusi vya ukimwi kwa kuweka mfumo bora utakaosimamiwa na serikali za Mitaa ili kuondoa mzigo wa kuhudumia wagonjwa kwa akina mama peke yao.
  12. Watanzania wote wenye kuishi na virusi vya ukimwi watapatiwa madawa {bure} na jamii kupitia serikali za vijiji na Mitaa na pia kupitia Asasi zisizo za kiserikali zitabeba jukumu la kuhudumia wagonjwa bila ubaguzi wa kijinsia.
  13. Tutatangaza malaria kuwa janga la kitaifa na tutoa huduma za afya kwa malaria bure.
  14. Huduma za afya zitatolewa bure kwa makundi maalum – waja wazito, vikongwe, wanafunzi, wenye kuishi na virusi vya ukimwi, watoto wachanga na walemavu

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl