lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MBUNGE KABWE HAWEZI KUOMBA RADHI, KAULI ZAKE NI ZA KWELI

  1. Maendeleo hayaletwi na CCM bali kodi za wananchi
  2. Kikwete aeleze anatumia fedha kiasi gani kwajili ya kazi za chama na kiasi gani kwajili ya kazi za serikali anapokuwa ziarani
Itakumbukwa kuwa Mei27, 2007. Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA, Kabwe Zitto alifanya mkutano na waandishi wa habari akiwaelezea kusikitishwa kwake dhidi ya uamuzi wa Rais Kikwete kuamua kutumia mikutano ya serikali kufanya shughuli za kisiasa.

Aidha kufuatia tamko hilo la Mh Kabwe Zitto, Leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Serikali imekanusha madai ya Kabwe Zitto na kudai kuwa Mh Kabwe Zitto anapaswa kumwomba radhi Mh Rais. .

Kutokana na ukweli kuwa wanaoathirika na mwenendo mbaya wa Rais Kikwete kufanya kampeni kwenye mikuytano ya kiserikali ni watanzania kwa ujumla wao. Walio na vyama na wasio na vyama. Na kwakuwa kauli hizo za kikada ambazo zimethibitishwa na serikali kupitia waziri wa habari na utamaduni zilitolewa na Rais akiwa katika ngome ya CHADEMA. CHADEMA kimeamua kutoa ufafanuzi na kutoa mwito kwa serikali kama ifuatavyo;

KUHUSU CCM KUSHINDA UCHAGUZI UJAO 2010 DHIDI YA CHADEMA.

Katika tamko la serikali. Serikali imethibitisha kuwa Kikwete alisema “Mmechagua mbunge wa CHADEMA, huo ni uamuzi wenu. Sisi tunajiandaa kushinda uchaguzi ujao”.

Kauli hii ni kielelezo kuwa, Rais wetu alikuwa anatoa ujumbe kwa wananchi wake kuwa halidhishwi wala hafurahii kata ile kuongozwa na upinzani. Na ndio sababu anaahidi(kwenye mkutano wa serikali) kuirejesha mikononi mwa CCM 2010 .

Kauli kama hii inapotolewa na Rais wa nchi katika mikutano ya serikali. inawafadhaisha wananchi walio wachagua viongozi wa upinzani katika maeneo yao kwa kutumia haki yao ya kikatiba.

CHADEMA tunasema, kauli hii ni ya kikada ambayo haikutegemewa kutolewa na kiongozi wa nchi anayeongoza watanzania wote bila kujali itikadi zao.CHADEMA tumezoe kusikia kauli hizo zikitolewa na watu jamii ya Makamba ambao ni viongozi wa chama katika mikutano ya chama.

Na sio kutolewa na viongozi wa serikali(Hasa mkuu wa nchi) katika mikutano ya serikali. Huu ni mfano mbaya kabisa kwa Rais anayetaka tuamini kuwa ana nia ya kustawisha demokrasia.Na kwakweli imetuhuzunisha sana.

HOJA KUWA VIONGOZI WA UPINZANI HAWAWEZI KULETA MAENDELEO.

Katika taarifa hiyo ya serikali, pia serikali imekiri Rais alisema kuwa “Hata mkichagua CHADEMA, dhamana ya kuwaletea maendeleo ni ya CCM kwa kuwa CHADEMA hakina serikali”

Hoja hii ilikuwa ilikuwa na lengo la kuonesha wananchi kwamba , Chama cha siasa kama CHADEMA hakiwezi kuleta maendeleo . Na hiki ni kielelezo tosha kuwa Rais aliupotosha umma na ilikuwa na lengo la kuwashinikiza wananchi wajiunge CCM kwa hoja kuwa ni CCM inyoaweza kuleta maendeleo na sio vinginevyo.

Kauli hii ni upotoshaji wananchi kwani kuna maeneo mbalimbali ambayo wamechagua upinzani na wamepata Maendeleo.

Pamoja na umasikini wao, Kigoma wanachagua CHADEMA kwasababu wameona matunda ya uongozi wa CHADEMA. CHADEMA kimeweza kuondoa tatizo la maji Karatu ambapo serikali chini ya CCM ilikuwa imeshindwa.

CHADEMA kimeondoa tatizo la Elimu ya msingi na sekondari Karatu ndani ya muda mfupi ambapo kila mwananchi anapata maji safi, Kila mwanafunzi aliyefikisha kiwango cha kujiunga sekondari anapata nafasi.

Hii ni tofauti kabisa na wialaya nyingi mno ambazo zinaongozwa na CCM.. Je, Yote haya Mh Rais Kikwete hawezi kuona kuwa ni matunda ya wananchi kuchagua upinzani?

Ni vema Mh Kikwete akatambua kuwa wananchi waliochagua viongozi wa CHADEMA Ligoma hawakukosea, ni watu wazima na ni watu makini wanaostahili kuheshimiwa kwa uamuzi wao.

Kwa miaka zaidi ya 30 ya CCM, Kigoma mjini ilikuwa na sekondari moja tu ya serikali. Lakini kwa miaka michache ya uongozi wa CHADEMA, Halmashauri ya Kigoma mjini imepiga hatua kubwa kimaendeleo.Na sasa kila mwanafunzi anayefaulu anapata fursa ya kusoma.

Na hata Kigoma kaskazini. Kazi anayofanya mbunge wetu kwa wananchi wake inaturidhisha. Kwa muda mfupi ameweza kuwatafutia wakulima wa kahawa soko la uhakika. Kitu ambacho mbunge wa CCM alikuwa ameshindwa kwa miaka mingi. Hata sekondari ambayo Kikwete aliifungua. Mbunge Kabwe Zitto alichangia tofali 20,000 na alikuwa mstari wa mbele kuunganisha wananchi waijenge bila kujali itikadi zao.

Yote hayo yatosha kuthibitisha kuwa kuali ya Mh Rais ilikuwa ya upotoshaji na yenye lengo la kisiasa tofauti na aina ya mkutano aliokuwa anahutubia.

KUHUSU KABWE ZITTO KUTOKUWEPO WAKATI WA ZIARA YA KIKWETE.

Itakumbukwa kuwa mwaka jana, Mh Rais aliunda tume ya kutafuta maoni ya wananchi kuhushu undaji wa shirikisho la Afrika Mashariki. Ambapo Mh Kabwe Zitto alikuwa miongoni mwa wateule wa Rais kuunda tume hiyo..

Na itakumbukwa kuwa wakati Mh Rais akiwa ziarani Kigoma. Mh Kabwe Zitto alikuwa akitimiza jukumu hilo Zanzibar. Hivyo madai ya Kikwete kushangazwa na kutokuwepo Kabwe Zitto katika mikutano yake ni kielelezo cha namna ama serikali yetu isivyo na mfumo mzuri wa taarifa kiasi kwamba Rais anaweza kusahau majukumu aliyowapatia viongfozi wake.

Au kama alikuwa anakumbuka, basi lengo la kauli ya Rais kusikitishwa na Mh Kabwe Zitto kutokuwepo kwenye ziara yake, lilikuwa kumchonganisha Kabwe Zitto kwa wananchi wake. Kitu ambacho kisingetegewa kuwa sehemu ya jukumu la Rais wa nchi.

MSIMAMO WETU

Kwanza, Mh Rais ameshauliwa vibaya kuhusu dhana ya maendeleo. Kudai kuwa maendeleo yanaletwa na CCM ni kupotosha. Maendeleo yanaletwa na kodi za wananchi bila kujali itikadi zao za kisiasa. CCM haina fedha kwajili ya maendeleo.

Pili, Mh Rais ameshauliwa vibaya kuhusu kazi ya Mbunge. Kazi ya Mbunge ni kuisimamia serikali itekeleze wajibu wake.Na wabunge wa upinzani wanaweza kufanya hilo.Kama anao ushahidi kuwa wabunge wa upinzani hawawezi kuleta maendeleo alete.

Tatu, Uchaguzi umeshakwisha tangu 2005.Inasikitisha leo mwaka 2007 kuona Rais anahoji busara za wananchi wa kigoma kuchagua upinzani.

Nne , kwakuwa Mh Rais ameamua kuchanganya ziara zake za kiserikali na kampeni za CCM, kiasi ambacho kinawafanya wananchi washindwe kutofautisha ziara zake na zile za Katibu Mkuu wa CCM, Makamba. Tunaomba sasa Mh Rais atueleze ametumia kiasi gani kwajili ya majukumu ya CCM akiwa katika ziara za serikali, na kiasi gani amekitumia kwajili ya majukumu ya kiserikali.

Mwisho, Kutokana na mwenendo huo. Tunapenda kutaarifu Umma kuwa hatuoni sababu za kwanini Mbunge wetu Mh Kabwe Zitto aombe radhi. Tunasisitiza kuwa Mbunge wetu hataomba radhi. Na badala yake Mh Rais ndiye anapaswa kuomba radhi kwa kutumia fedha ya walipa kodi wa nchi hii(walio wana CCM, Wa vyama vingine na wasio na vyama) kufanyia kampeni za CCM.

Imetolewa 29/5/2007:

Erasto Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi


 
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl