|
|
|
|
|
|
|
TAMKO LA WAKUU WA VYAMA JUU YA USHIRIKIANO WA VYAMA VYA SIASA VYA UPINZANI TANZANIA
SABABU ZA USHIRIKIANO WA VYAMA VYA SIASA VYA UPINZANI TANZANIA
Vyama vinne vya Upinzani CHADEMA, CUF, NCCR – Mageuzi na TLP viliainisha mambo yafuatayo kama msukumo na sababu za msingi za kuanzisha Mashirikiano:
- Mara nyingi suala la mashirikiano ya vyama limekuwa likizungumziwa pindi uchaguzi unapowadia au kwenye matukio maalum na hivyo kufanyika katika hali ya kurashiarashia na isiyokuwa ya umakini wa kutosha na hivyo kutofaulu malengo yetu.
Jambo hili likianzishwa hivi sasa utakuwa ni wakati muafaka kwani tunao muda wa kujiandaa na kujipanga ( miaka 3 ) kabla ya Uchaguzi ujao.
- Tangu 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa rasmi malengo makuu ya vyama vya Upinzani ya kuchukua dola au kuwa na sauti katika kuathiri (influence) maamuzi ya serikali iliyoko madarakani bado hayajawa na nguvu inayopasa hadi sasa. Na mbaya zadi, kadri muda unavyopita nguvu hiyo imekuwa ikionekana kitaswila kupungua.
- Wapinzani kutoshirikiana kumekuwa kukiwafanya CCM WASHINDE KATIKA Chaguzi mbali mbali kirahisi kutokana na kutokuwepo kwa nguvu ya pamoja ya kukabiliana na hujuma za Chama Tawala wakati wa Uchaguzi.
- Hali halisi imedhihirisha kuwa kadiri muda unavyopita CCM imeendelea kujiimarisha zaidi kupitia nguvu za mtandao haramu wa kidola na kuzidi kuvidhoofisha vyama vya upinzani na kuhakikisha taswira hiyo inaonekana hivyo kwa umma, ili visiheshimike, kutumainiwa wala kuaminika. Kwa kiasi kikubwa CCM imefanikiwa na inaendelea kufaulu kwa kasi katika jambo hili linalofanyika kwa njia zilizo chafu.
Kwa Zanzibar ambako upinzani mkubwa na kushindwa kwa CCM kumekuwa dhahiri zaidi, CCM wameendelea kujenga na kutengeneza mazingira ya wazi ya kupora Ushindi kwa nguvu.
- Kutokana na kutokuwa na mashirikiano ya pamoja, kauli na mipango ya kutufitinisha, kutuchonganisha, na kutuhujumu kama wapinzani imekuwa ikifanya kivyepesi na CCM na vyombo vyake vya dola kupitia kwenye vyama vyetu ka njia mbali mbali zisizoweza kugundulika kirahisi.
- Watanzania walio wengi wamekuwa wakielezea wazi umuhimu wa upinzani kushirikiana na kujenga nguvu ya pamoja ya kulikabili “CHAMA DOLA CCM”. Wengi wanaona kuwa ushirikiano wa upinzani katika mazingira ya sasa ya kisiasa ndilo jibu pekee, na kutofanya hivyo ni kuzidi kuwakatisha tamaa na kuwachanganya wananchi hali itakayopelekea kuwafaya wasiwe na matumaini na upinzani.
- Viongozi wetu wameona kuna haja ya kusoma alama za nyakati za mwenendo wa kisiasa. CCM wamekuwa wapesi kulitambua hilo na wamekuwa wakijibadilisha kama kinyonga kwa kutegemea upepo na mtizamo a kisasa na hali ya mazingira yaliyopo ili mradi wakidhi haja yao ya kuendelea kuwepo madarakani hata kama utawala wao hauna ufanisi wa tija. Mwenendo wa siasa za sasa zilivyo si vyema kuendelea kuendekeza na kutanguliza umimi bali tuangalie ni lipi la kutufanikishia njia tunayoihitaji sasa.
- Vyama vya Upinzani vina rasilimali yenye ufahamu na kuaminika ya “RASILIMALI WATU” ambayo imesambaa bila utaratibu ulio mzuri na makini wa kuiratibu na kuitumia. Kugawanyika na kutawanyika kwa rasilimali hiyo muhimu kunaifanya isiwe thabiti (effective) pale ilipo na CCM kunufaika na hali hiyo.
- Kutokana na kukosekana nguvu ya pamoja iliyo kubwa, upinzani umeshindwa kutoa msukumo wenye nguvu hata wakati wa kuwasilisha madai yenye msingi ambayo yangepaswa kusikilizwa na kufanyiwa kazi na Serikali. Mfano; madai ya Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi matatizo ya sheria mbovu na utaratibu usioridhisha unaosimamia chaguzi, ukiukwaji wa haki za binadamu, tatizo la Zanzibar n.k.
- Kutokana na kukosekana ushirikiano wa pamoja wa Vyama Vya Upinzani katika kuunganisha nguvu ya Umma kuwawajibisha Viongozi na Serikali iliyo madarakani kutekeleza ahadi lukuki ilizozitoa na inazoendelea kuzitoa pamoja na kushirikiana katika kukabiliana na rushwa, umaskini, ujinga na maradhi.
|
| |
 |
 |
|
 |
 |
|
|
|