Kutambua, kulea na kuandaa viongozi wa baadaye wa serikali na chama kwa kuwajengea uwezo wa kiuongozi na kitaaluma.
- Katika kipindi cha miaka mitano mafunzo yatapewa kipaumbele katika maeneo mbalimbali.
- Kutambua,kujenga mawasiliano na kuwaandaa wagombea watarajiwa mapema na Kuhakikisha chama kinashinda katika chaguzi ndogo zitakazojitokeza hususani katika ngazi ya ubunge.
- Kuhamasisha vijana kujiunga na CHADEMA, wengine kugombea uongozi na mkazo utawekwa katika kuwapa vijana mbinu na mafunzo ya kisiasa hususani katika ngazi za chini.
- Mkazo uwekwe kuhakikisha wanawake wengi wanajiunga na CHADEMA na kuandaliwa kupenya katika uongozi na kuwa mhimili muhimu wa chama wakati wa chaguzi mbalimbali.