Kupanua na kujenga ofisi ya Makao Makuu ya chama kwa kuongeza vifaa na uwajibikaji ili kuongeza hadhi, ufanisi, tija na utekelezaji wa shughuli na maamuzi ya vikao vya chama:
- Idara ya raslimali itahusika na kutambua, kubuni, kusimamia na kupata raslimali za chama mathalani fedha, miradi, vifaa, muda, mawazo na nyenzo nyingine toka kwa wanachama, wapenzi wa chama na wadau wengine wa maendeleo.
- Kuwekeza katika uzalishaji (bila kukifanya chama kifanye biashara). Kuendesha michango ya umma (local fundraising) kwa kutumia shughuli za namna mbalimbali.
- Idara ya Fedha itahusika na usimamizi wa matumizi ya fedha kwa pamoja na mambo mengine kuandaa kanuni za mapato na matumizi ya raslimali/fedha na kuhakikisha zinafuatwa katika ngazi mbalimbali za chama.
- Ofisi ya Mwenyekiti wa Taifa itatafsiriwa kuwa ni pamoja na Makamu Wenyeviti wa chama. Ofisi ya Mwenyekiti Taifa itapatiwa watendaji ili kusaidia kuongeza ufanisi na kuitaasisisha (instutionalize) ofisi hii muhimu sana kwa chama.
- Kuimarisha ofisi ya makao makuu Zanzibar kutawekwa kipaumbele kama suala la msingi.