Kutafiti, Kuibua na kuboresha sera za chama na kuzitangaza ili zifahamike na kukubalika kwa jamii.
- Kufanya ziara za mara kwa mara ili kuhakikisha chama kinaenea hususani katika maeneo yanayolengwa.Kuhakikisha viongozi wanaohusika na uenezi katika ngazi za chini wanajengewa uwezo na kuimarisha mchakato mzima wa upatikanaji na usambazaji wa habari.
- Kutekeleza mikakati mbalimbali ya kujipenyeza katika vyombo vya habari vilivyopo na ikiwemo kutafakari kuanzisha chombo cha habari cha chama.
- Kuadhimisha siku muhimu za chama.
- Kuzindua upya chama kutakakotanguliwa na kubuni alama mpya za chama bila kupoteza utambulisho wa muhimu wa chama.
- Kuwekeza katika kuwaeleza wananchi sera mbadala kwa upande mmoja lakini pia kufanya mikakati ya kuchambua mapungufu na kuyaweka wazi mapema ili wananchi wapate sababu ya kuzikubali sera mbadala zinazotolewa.
- Pia mkazo utawekwa katika kueneza yake ambayo yamefanyika kutokana na sera au msukumo wa upinzani hususani CHADEMA ili wananchi waweze kuthibitisha umuhimu wa upinzani na haja ya kufanya mabadiliko ya mfumo mzima.
- Hivyo matumizi ya vyombo vya habari na mtandao wa chama katika kufanya uenezi na propaganda lazima yapewe kipaumbele.
- Idara ya sera na utafiti itafanya utafiti kuwa suala mtambuka (cross cutting) ili kuwezesha kurugenzi mbalimbali na viongozi wa chama kupata masuala muhimu kwa kadiri ya mahitaji;Kwa upande mwingine,ufuatiliaji utafanyika kubaini utekelezaji wa ahadi za serekali (peformance tracking).
- Sera ya CHADEMA kuhusu Muungano iwe msingi muhimu wa mwelekeo wa chama kuhusu masuala ya Zanzibar.
- Kuendeleza dhana ya mbadala wa tatu (third alternative) kama njia ya kukijenga CHADEMA Zanzibar.