Kushirikiana na vyama vya kiraia katika kutoa elimu ya kisiasa kwa wananchi ili kuongeza uelewa na haki zao na kuwawajibisha viongozi wao.
- Mkazo utawekwa katika kutoa mafunzo kwa viongozi na wanachama kuanzia ngazi ya chini. Pia mkakati wa kuhamasisha chama kuwa serekali mbadala katika maeneo ambayo chama hakijashinda utafanyika kama inavyodokezwa katika masuala ya sera na sheria.
- Kuhakikisha kuwa chama kinaendeleza asasi/taasisi ambayo itaweza kutekeleza programu mbalimbali za demokrasia na maendeleo, mathalani: Kujiunga na mitandao sambamba na kushirikiana na mashirika mengine ya kiraia ya kitaifa na kimataifa; Kutoa elimu ya kisiasa, mafunzo kwa viongozi pamoja na kuunganisha nguvu za kidemokrasia/kimaadili nk.