lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Jihusishe
»Jiandae kwa 2009
»Jiandae kwa 2010
»Ilani ya 2005
»Utekelezaji wa Ilani
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Kura za Awali
»Gombea Ubunge
»Gombea Udiwani
»Jiunge Uanachama
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Matamko ya Chama
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
»Katuni
b.part


Waraka Namba 1 wa Mwaka 2000

KUHUSU WAGOMBEA UDIWANI, WAGOMBEA UBUNGE WA VITI MAALUM, UBUNGE WA KUTEULIWA NA RAIS KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WAGOMBEA UBUNGE KATIKA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

1.0 Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na.1 wa Mwaka 2000 uliwekwa Masharti yanayowaongoza Watumishi wa Umma kushiriki katika shughuli za Kisiasa nchini.

2.0 Baada ya Masharti hayo kutumika kwa muda wa takriban mwaka mmoja na nusu, Serikali imeamua kufanya marekebisho katika Waraka huo kwa lengo la kuboresha Masharti hayo kwa Watumishi wa Umma watakaoamua kugombea au watakaoteuliwa katika nafasi zilizotajwa hapo juu kama ifuatavyo:

2.1 Watumishi wa Umma wanaoamua kugombea Udiwani

Watumishi wa Umma watakaoamua kugombea Udiwani wanaruhusiwa kufanya hivyo na endapo watabahatika kushinda wataendelea na ajira zao kwani Udiwani sio ajira.

Hata hivyo Watumishi wa Umma ambao ni waajiriwa katika Halmashauri (Council) hawaruhusiwi kugombea Udiwani katika Halmashauri wanazofanya kazi.

2.2 Watumishi wa Umma Wanaoamua Kugombea Ubunge Kupitia Viti Maalum

Watumishi wa Umma watakaoamua kugombea Ubunge kupitia Viti Maalulm wanaruhusiwa kufanya hivyo na endapo watashindwa wana hiari ya ama kuacha kazi na kulipwa mafao yao au kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote cha uhai wa Bunge tangu Tume ya Uchaguzi itakapowatangaza kuwa Wabunge.

2.3 Watumishi wa Umma Wanaoteuliwa na Rais wa Kuwa Wabunge kwa Mujibu wa Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (Toleo la Mwaka 2000)

Watumishi wa Umma watakaoteuliwa na Rais kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Toleo la Mwaka 2000) wana hiari ya ama kuacha kazi na kulipwa mafao yao au kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote cha uhai wa Bunge kuanzia siku watakayoteuliwa.

2.4 Watumishi wa Umma Watakaogombea Ubunge Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki

Watumishi wa Umma watakaochaguliwa kuwa Wabunge katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaweza kuendelea na kazi katika Utumishi wa Umma au kuchukua likizo bila malipo. Aidha, wakati wa kuhudhuria Vikao vya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watalazimika kutoa taarifa kwa Waajiri wao na watapewa ruhusa maalumu ya kuhudhuria Vikao hiyvo.

3.0 MWISHO

Masharti mengine yanabaki kama yalivyo. Aidha, marekebisho haya yatatumika kuanzia tarehe ya Waraka huu; Isipokuwa kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Afrika Mashariki marekebisho haya yatatumika kuanzia tarehe 15 Juni, 2001.

Hili ni Rekebisho Namba 1 la Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Uliyotolewa mwaka 2000 na M.Y.C. Lumbanga, Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl