lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Ijue CHADEMA
»Utangulizi
»Falsafa ya Chama
»Itikadi ya Chama
»Uanachama
»Viongozi wetu
»Historia ya CHADEMA
»Jiunge Uanachama
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Ijue CHADEMA

Utangulizi

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama mbadala kinachokua na kinachoongozwa kwa Falsafa ya “Nguvu ya Umma” na kuamini katika itikadi ya “Mrengo wa Kati”. CHADEMA inawataka watanzania kuelewa kwamba mabadiliko ya kweli yataletwa na kubadilisha mfumo wa utawala. Maendeleo ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi walewale wa chama kile kile chenye uoza ule ule wakiendeleza yale yale kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. CHADEMA inatambua kwamba kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema (CCM), Tanzania yenye neema kamwe haitawezekana. Lengo la CHADEMA ni kusimamia mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli ili kuunda Taifa la watu walio huru na lenye kuzingatia misingi ya utawala bora na linalotoa fursa kwa wananchi wake kushiriki katika kuboresha maisha yao. Tanzania endelevu, yenye haki na isiyovumilia ukandamizaji wa aina yeyote kwa wananchi wake-ndiyo nchi tunayoitaka. CHADEMA inafanya kazi kuhakikisha kuwa vyombo vya utawala na viongozi wanafanya maamuzi ya busara na makini yanayowaletea wananchi nafuu ya maisha na kuwapa matumaini ya kuendelea kupiga hatua za kimaisha katika nyanja zote za maendeleo.


Chama kimezinduliwa Upya?

Agosti 13, 2006 Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilizinduliwa Upya. Ilikuwa siku ya kipekee na muhimu sana katika historia ya Chama.  soma zaidi


Nini Falsafa ya Chama?

Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.  soma zaidi


Chama kina Itikadi gani?

CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).  soma zaidi


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl