lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Utangulizi

Oktoba 21, 2006 CHADEMA kilizindua mchakato wa kukusanya maoni ya vijana na wadau mbalimbali kuhusu Sera ya vijana ya CHADEMA ili kuifanya sera hii iendane na mahitaji ya sasa. Pia baadhi ya mambo yaliyopo katika sera ya sasa na kutoa maoni yako kwa lengo la kuboresha sera hii ya vijana. Mwisho wa kutoa maoni yako ni Januari 30 mwaka 2007:

Sera ya Vijana ya CHADEMA

Masikini Vijana wa Tanzania, kwa nini lakini?

  1. Vijana, wasichana na wavulana ni sehemu kubwa ya Taifa – zaidi ya nusu ya Watanzania wote.
  2. Vijana bado wanaonekana ni Taifa la kesho.
  3. Vijana wanatumiwa kama washabiki katika siasa - ushiriki wao katika uongozi ni finyu.
  4. Ukosefu wa ajira kwa vijana unazidi kuongezeka – Hasa vijana wa kike hawana ajira na kujikuta wanajiingiza katika vitendo vya biashara ya ngono.
  5. Vijana wenye vipaji wametelekezwa – vipaji vya vijana haviendelezwi.
  6. Vijana wengi ni hohehahe – vijana wako duni zaidi kiuchumi.
  7. Vijana wanabugudhiwa – wanakamatwa kwa uzururaji, wafanyabiashara ndogondogo wanatimuliwa!
  8. Vijana wanateketea kwa UKIMWI na madawa ya kulevya.
  9. Michezo imepuuzwa na vijana hawana cha kufanya hivo kujiingiza katika uhalifu.

Serikali ya CHADEMA na sura mpya ya Vijana wa Tanzania

  1. Tunaamini kwa vitendo kuwa kijana ni Taifa la Leo.
  2. Tutatoa fursa na kuwezesha kizazi kipya kuwa mstari wa mbele katika siasa, uchumi na sekta nyingine.
  3. Tutaweka mazingira ya kuundwa kwa Baraza Huru la Vijana Tanzania.
  4. Tutawezesha vijana wa kike na wa kiume kumiliki ardhi na rasilimali nyingine kwa kutenga maeneo kadhaa ya biashara kwa vijana tu.
  5. Tutaweka kipaumbele katika kukuza ajira kwa vijana kupitia vipaji vyao katika nyanja mbalimbali – tutazielekeza halmashauri kuanzisha mifuko ya ukuzaji vipaji vya Vijana.
  6. Tutaweka mazingira ya kuboreshwa kwa malezi ya Vijana katika familia na mashuleni ili kukabiliana na UKIMWI na madawa ya kulevya.
  7. Tutatoa leseni za bure na likizo ya kodi kwa Vijana wafanyabiashara ndogondogo na Vijana wanayojishughulisha na uzalishaji mali.
  8. Muziki wa kizazi kipya utapewa kipaumbele ili soko la muziki huu litakuzwa nje ya Tanzania.
Asante kwa kupitia maeneo ya sera ya vijana ya CHADEMA inayohitaji kuboreshwa. Tafadhali tuma maoni yako kwenye anuani pepe vijana@chadema.net ama sanduku la posta 31191, Dar es salaam.Vijana: ”Nguvu ya mabadiliko”

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl