Makala za Mwenyekiti Mstaafu
13 Machi 2008
Tuimarishe Demokrasia tuepuke Ufisadi
"...Mjadala uliozuka Tanzania kuhusu ufisadi hivi karibuni, ambao ulipelekea kuundwa kwa Baraza la Mawaziri upya, Mhe. Mizengo Pinda akiwa ni Waziri Mkuu, umedhihirisha umuhimu wa kutathmini kwa kina Katiba ya nchi yetu na sheria zinazohusu ubunge na vyama vya siasa. Nitajieleza kidogo...."
19 Februari 2008
Ufisadi huu unatisha
"...NIMESOMA muhtasari (Executive Summary) wa Ripoti ya Kamati Teule ya Richmond na nilipata pia fursa ya kumsikiliza Mhe. Harrison Mwakyembe alipokuwa anaiwasilisha bungeni, licha ya kwamba umeme hapa kwetu ulikuwa unakatika katika kama kawaida..."
29 Januari 2008
Tunakosa washauri wa uchumi na fedha?
"...Matamshi na maamuzi ya serikali ya hivi karibuni, yanaashiria ama hatuna washauri wa kiuchumi na fedha au tunapuuza ushauri huo. Nitatoa mifano michache:
Vyama vya wafanyakazi vikiongozwa na wakuu wao walitangaza kwamba walitaka kiwango cha chini cha mshahara kiwe sh 315,000 kwa mwezi..."
16 Januari 2008
Uchaguzi wa Kenya: Tanzania tujifunze nini?
"...Katiba ya Tanzania inafanana fanana na ile ya Kenya, kwa vile zote mbili zinaruhusu vyama vingi vya siasa. Hata Tume ya Uchaguzi ni hivyo hivyo. Zote zinateuliwa na rais, na licha ya kwamba sisi Tanzania tunatamka kwamba tume ni lazima iwe huru, ubinaadamu unakuwepo, hasa pale Watanzania wengi, kama Wakenya, hawataki “kumwaga unga”. Wakina Kivuitu, Masauni na watu kama hao, wamezagaa kila kona!..."
26 Desemba 2007
JK anashauriwa vibaya kuhusu rushwa, uzembe
"...Rushwa na uzembe unaowahusu viongozi na wakubwa, hautadhibitiwa Tanzania kama Rais Jakaya Kikwete ataendelea kuchukua hatua kama anavyoshauriwa sasa.
Na jinsi rushwa na uzembe wa wakubwa unavyoota mizizi na kuenea nchini, ndivyo dhiki na umaskini vitakavyoshindikana kutokomezwa hapa nchini na imani kwa rais wetu itakavyoendelea kupungua..."
11 Septemba 2007
Nilipinga, naendelea kuipinga mikataba ya siri
"...Hata ile niliyosaini nikiwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki haikuwa ya siri. Ni jambo la kusikitisha kwamba RAI katika toleo la Alhamisi la Septemba 5, linamaanisha kama vile nimebeza msimamo wa Mheshimiwa Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Chama chetu cha CHADEMA juu ya jambo hilo..."
19 Juni 2007
Marekebisho ya Katiba nchini hayaepukiki (6)
"...Sheria yetu inayosimamia Zabuni za Serikali (Public Procurement Act) inatamka bayana kwamba ofisa yeyote anayehusika na uchambuzi wa zabuni, ni lazima ajitoe kama ana uhusiano kibiashara au kifamilia na mzabuni yeyote. Sasa kama rais atakuwa mfanya biashara na huku ndiye ‘msimamizi’ wa zabuni zote za serikali, kwa maana kuwa anaweza kufuata au kuagiza mabadiliko katika maamuzi ya serikali, atawezaje kusimamia shughuli ya umma?..."
5 Juni 2007
Marekebisho ya Katiba nchini hayaepukiki (5)
"... Wakati huo, katiba ilikuwa inatamka kwamba, mgombea kuchaguliwa ni lazima apate kura za “NDIYO” zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa. Vinginevyo, chama kingelazimika kuleta mgombea mwingine. Tulipopata demokrasia ya vyama vingi, mwaka wa 1992, katiba ilibadilishwa na kutaka “Mgombea yeyote wa kiti cha rais…apate zaidi ya nusu ya kura zote halali zilizopigwa.” La sivyo, uchaguzi ungerudiwa ....."
29 Mei 2007
Marekebisho ya Katiba nchini hayaepukiki (4)
"... Rais pia ndiye mwenye kauli ya mwisho juu ya maaumuzi muhimu ya mhimili wa kutunga sheria (Bunge), kwa maana kwamba ni lazima rais akubali na kuridhia muswada uliopitishwa na Bunge kabla haujawa sheria. Katiba inampa pia rais uwezo wa kutoa msamaha au kupunguza makali ya maamuzi ya Mahakama Kuu kama mhimili wa kutoa haki....."
11 Mei 2007
Marekebisho ya Katiba nchini hayaepukiki (2)
"...MAPENDEZO yangu katika mgawanyo wa wabunge Tanzania Bara, wabunge wa majimbo wachaguliwe 150, wabunge wanawake viti maalum wawe 75, wabunge wa uwiano wa kura za vyama wawe 75.
Tanzania Zanzibar; wabunge wa majimbo wachaguliwe 28, wabunge wanawake wa viti maalum wawe 14 na wabunge wa uwiano wa kura za vyama wawe 14...."
8 Mei 2007
Marekebisho ya Katiba nchini hayaepukiki
"...TANGU Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania irekebishwe, kuzingatia uwepo wa vyama vingi vya siasa, mwaka 1992, kumekuwa na ubishi au majadiliano kwamba Katiba iandikwe upya, na kwamba ‘viraka’ vya kila mara katika Katiba yetu vimezidi.
Hata hivyo, hakuna chama chochote cha siasa ambacho kimeorodhesha kinaga ubaga kwamba ni kasoro gani zingezingatiwa endapo ingekubalika kwamba Katiba iandikwe upya...."
3 Mei 2007
Mita zitumike kulipia ushuru wa kuegesha magari
"...Kama kila manispaa ikijiwekea kiwango, tutaweza kuwa na gharama zisizokuwa na sababu, ambazo wale wanaoegesha watazitafutia njia za kuzifidia. Kama ni wafanyabiashara labda wataongeza bei ya bidhaa wanazouza n.k. na umma utaathirika. Hakuna tofauti na kodi nyingine, na ni lazima tuondoe uholela wa kutoza aina hii ya kodi. Pia ni lazima serikali iweke utaratibu wa kisheria wa jinsi ya kukusanya ushuru huu..."
3 Aprili 2007
Siwaelewi kuhusu rushwa ya rada
"...LAZIMA nikiri kwamba sielewi msimamo wa viongozi wa Tanzania kuhusu rushwa iliyolipwa wakati serikali yetu iliponunua rada iliyotugharimu dola za Kimerikani milioni 41 badala ya bei yake ya kawaida ya dola milioni 28. Tumeelezwa na rais wetu kwamba, Serikali ya Uingereza ilikubali kuidhinisha kampuni ya nchi hiyo iiuzie Tanzania chombo hicho kinachotumika kwa ulinzi wa kitaifa..."
10 Februari 2007
Rushwa ya kamisheni inavyolipwa
"...KATIKA majadiliano juu ya rushwa ya wakubwa, niliyoshiriki hivi karibuni, ilionekana watu wengi hawajui mbinu za kawaida zinazotumika kupokea au kulipa rushwa baina ya wakubwa. Nimeamua kuandika makala hii kwa lugha nyepesi ili umma ufahamu mazingira yanayotuzunguka..."
2 Februari 2007
Tujiamini, vinginevyo maendeleo yatakuwa duni
"...Sasa inaonekana kuna kasumba iliyoenea miongoni mwa Watanzania kwamba hatuwezi kuendesha lolote. Hatujiamini tena. Hasa viongozi wetu wakuu hawana imani na wasomi wetu, licha ya miaka 45 ya uhuru ambayo imeshuhudia kuongezeka kwa wataalamu wa kikwetu kwa zaidi ya mara mia moja..."
|