Makala za John Mnyika, Mkurugenzi wa Vijana
26 Juni 2008
Hatma ya Richmond/Dowans - "Ni wakati wa kuchukua hatua"
Februari 6 mwaka 2008 Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa tarehe 13 Novemba, 2007 iliwasilisha taarifa yake bungeni. Kamati hiyo iliundwa kuchunguza mchakato wa Zabuni ya Uzalishaji umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas Marekani mwaka 2006...
2 Machi 2008
Lowassa hawezi kuiepuka Richmond
NIMEFUATILIA kauli za kujitetea za hivi za Edward Lowassa, Mbunge wa Monduli. Nimeshangazwa na jitihada zake hizo kwa sababu zimezidi kumchafua. Lowassa amenishangaza kwa ujasiri alio nao wa kuthubutu kujitokeza hadharani na kujitetea kuhusu kuhusika kwake katika kashfa ya Richmond...
2 Juni 2007
Tanzania, CHADEMA, CCM na mjadala wa falsafa na itikadi; Lipi ni jibu?
Mwalimu Julius Nyerere alitamka wazi kwamba CCM haifuati siasa ya ujamaa na kujitegemea, "Halmashauri Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi. Na walikuwa na haki ya kufanya hivyo, maana sera ni yao, ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na hadi sasa wanaendelea kuwadanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea"...
26 Mei 2007
Msolla 'hola!', Lowassa 'anakula', Wanafunzi Ukraine 'wanalilia' chakula; Wewe je?
Hivi ni mzazi gani ambaye akipigiwa simu, akiambiwa mwanae yuko ugenini - hana pa kulala, hana pakula; yuko ana waya waya kwenye mageti ya majirani- atajibu nakula! Ama atasema waulizwe ndugu wengine au ataka kabisa simu? Jibu unalo wewe...
26 Mei 2007
Ushirikiano wa Upinzani na hekima ya Umoja ni Nguvu
Lengo letu kuu na la pamoja na la jumla ni kuunganisha nguvu zetu katika kukabiliana na mfumo wa chama dola uliopo sasa ambao umezuia kukua kwa demokrasia, ukiukwaji wa haki za msingi za raia, kuongezeka kwa ukandamizaji , rushwa, vitendo vya ufisadi na kuzorota kwa uchumi. Pili, vyama vyetu vitafanya kazi au kuendesha shughuli zake za kisiasa kwa pamoja na kushauriana katika masuala yote makuu ya kisiasa, ya kuichumi na ya kijamii katika Tanzania...
19 Mei 2007
Richmond na utetezi wa TAKURU
TAKURU kuisafisha kampuni ya Richmond: “...Hakuna ushahidi wowote uliopatikana kuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe na upokeaji wa kamisheni kwa watendaji wa serikali… uchunguzi huo umethibitisha udhaifu wa kawaida katika utendaji na ambao haukuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyote ile kwa upande wa watendaji na hakuna hasara iliyosababishwa na udhaifu huo...Baada ya kuona hivyo, Richmond ilionekana kufahamu mwenendo wa mambo serikalini”...
21 Aprili 2007
'Sera ya Majimbo': Afrika Kusini, Nigeria na mfumo mpya wa utawala Tanzania
Nafurahi kwamba kuna waliopingana na hoja zangu si kwa sababu tu ya kubisha, ila wameingia katika viatu vya watanzania wenye hofu kuhusu majimbo ama wanaopotoshwa kuhusu majimbo. Na ni kweli kabisa. Na hasa baada ya kuzindua sera ‘nzito’ (heavy) kwenye uchaguzi na tena kuanzia kuitambulisha Kilimanjaro!...
14 Machi 2007
'Sera ya majimbo' ni siri ya maisha bora kwa kila Mtanzania
Suala la sera ya majimbo ni suala la kikatiba. Chama chochote cha siasa kinauza kwa wananchi matakwa yake kama kikipewa ridhaa na wananchi. Matakwa hayo yanaweza kutokana na misingi ya chama husika ama matakwa ya wananchi ama matakwa ya viongozi wa chama husika. Lakini baada ya uchaguzi zipo sera ambazo utekelezaji wake lazima urudi tena kwa wananchi kupata ridhaa ya pamoja...
6 Februari 2007
Kikwete anacheza na vichwa vya wasomi
Rais Kikwete amenukuliwa akisema, atalipatia ufumbuzi suala la wanafunzi kuchangia asilimia 40 na kwamba hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kusoma kutokana na kutakiwa kulipia kiasi hicho. Hizi ni propaganda za kisiasa kwa kuwa wakati rais anatamka maneno haya, tayari wapo wanafunzi wa vyuo mathalani, Tumaini, ambao wamezuiwa kufanya mitihani na hivyo kushindwa kuendelea na masomo...
1 Februari 2007
Suluhisho la migomo ya wanafunzi ni kutenda haki
Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla, amenukuliwa na vyombo vya habari akitoa vitisho kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa madai kuwa wanafunzi wanaohusika na migomo katika vyuo vikuu wanajiandalia mikosi na kwamba hawatapata ajira baada ya masomo yao...
9 Disemba 2006
45th Anniversary: My greetings to you and reflections with Mwalimu Nyerere
Today is our day. For millions of Tanzanians today is the celebration of the Independence Day. We are joining our hearts regardless age, gender, color, origin and tribe to mark the day we were freed from direct colonialism. But I do not believe if we should celebrate!...
10 Oktoba 2006
"Vihiyo" na Hatma ya Tanzania
Vihiyo! Ni wakina nani? Kamusi niliyonayo hainipi tafsiri ya neno hili. Lakini kumbukumbu zinaniambia Mwaka 1996 aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Temeke kupitia CCM Bw. Ramadhani Kihiyo, alibainika kughushi vyeti vya elimu, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, mahakama ikatengua matokeo ya uchaguzi....
1 Septemba 2006
Chambelecho cha maadhimisho Siku ya Mashujaa: Tunu yangu kwa Kinjeketile
Kamaradi Kinjeketile na mashujaa wenzako popote mlipo! Hii ni tunu kwenu. Hidaya kwenu mliomwaga damu wakati mapambano kadhaa na Mreno na Mwarabu. Tuzo kwenu nyinyi mliopigana na Ujerumani wakati wa utawala na mliomwaga damu katika vita vya dunia. Heko ninyi ambao damu ilisafisha safari ya kumng’oa Nduli Amin. Heri wewe Sethi Benjamini...
2 Julai 2006
“New vigor, energy and speed” is needed to invigorate the role of civil society
“Power corrupt and absolute power corrupts absolutely”. This historical dictum lays a basis in good governance theory and practice for governments to be controlled. Such control ranges from criticism to compliment. This is spearheaded by individuals and institutions of various kind...
5 Aprili 2006
Asante Waziri Sitta, Usisite kuchukua hatua
"...CCM kwa upande wake haikuwa na suala hili katika ilani yake lakini Rais Jakaya Kikwete ametamka hadharani kwamba hili ni moja ya suala ambalo kila alipopita wakati wa kampeni wananchi walimwomba alishughulikie..."
7 Machi 2006
Watchdog or toothless civil society?
"...Benjamin Mkapa who was committed to strengthen institutions on one hand but a staunchest advocate of pocketing them on the other. Civil society organizations that maintained their stand were either deregistered as it was for National Youth Forum (NYF) or mouth-taped as it happened to HakiElimu..."
|