lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
»Hotuba za Mnyika
»Makala zingine
»Habari Mpya
»Matamko ya Chama
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
»Katuni
b.part
Barua Pepe
   
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Makala za John Mnyika, Mkurugenzi wa Vijana

25 Februari 2006     
Tamko la JJ kuhusu mchakato wa Uchaguzi Ubungo
"...Kupitia kampeni zangu nimedhihirisha kuwa vijana ama wananasiasa wa kizazi kipya wanao uwezo kabisa wa kushika mamlaka katika nchi hii. Imedhihirika pia hata bila ya rushwa na takrima upo uwezekano wa mgombea kukubalika katika jamii..."

19 Februari 2006     
Waziri Rita Mlaka alidanganya Bunge
"...Ninashindwa kuelewa waziri huyu anamaanisha nini kwa kusema ofisi yake haijapata barua hiyo? Kama barua imefika mlangoni mwa ofisi yake na kupokewa na sekretari wake, nakala ikapelekwa pia masijala na kupokelewa, sasa ifikishwe wapi hata ionekane imefika ofisini kwake? Au ofisi ya naibu waziri inaanzia wapi?..."
2 Novemba 2005     
Kikwete: Mafiga Matatu-ndio!, lakini...
"...Mpiga kura makini anapaswa kuchangua kiongozi bora ili apate maendeleo. Kikwete anakiri kabisa kuwa mafiga yake ni mabovu. Vipi amlazimishe Mpishi kuyapikia? Ndio maana nasema nakubaliana na hoja ya mafiga matatu kama zana ya kukibeba chungu cha maendeleo. Mpishi makini akikosa mafiga bora ndani ya nyumba yake anatoka kwenda kutafuta na akikosa huazima kwa jirani..."
22 Oktoba 2005     
Upanuzi wa barabara uzingatie Sheria na Haki
"Hii ni kutokana na ukweli kuwa kila raia anaamini kuwa serikali anapaswa kufahamu sheria kuliko raia. Serikali isiyo fahamu au isiyosimia sheria haifai! Kwani kwa vyovyote vile haiwezi kuongoza kwa msingi wa utawala wa sheria ambao ndio muhimili muhimu wa utawala bora..."
4 Septemba 2005     
Kombe la Dunia kutembezwa Tanzania
"Tumepiga hatua katika Soka? ...Kauli hivi karibuni za Kapuya ambae kimsingi ni kauli za serikali haitofautiani na ile iliyowahi kutolewa na rais wetu, Mheshimiwa sana Ben Mkapa wakati wa ziara ya aliye kuwa rais wa Marekani Bill Clinton mkoani Arusha, rais wetu alisema, "Ukiona Clinton anakuja Tanzania ujue uchumi umekua"!..."
2 Juni 2005     
Makamba huu ni Undumilakuwili
...Quran Tukufu Surah ya pili Al-Baqarah aya 188 inasema usile kwa mali ya mwingine bila ya haki wala usitoe hongo kwa mtawala. Nayo Biblia Tukufu inatamka "Nawe usipokee rushwa, kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki (Kut:23:8)..."
5 Aprili 2005     
J.J. ajibu mapigo ya Makamba
"...Hii inadhihirisha hoja yangu kwamba uongozi ulisinzia miaka yote hiyo na kukurupuka majuzi ukiwa na nia ya kulaghai wapiga kura. Napenda kumkumbusha Makamba kwamba usingizi wa viongozi wenzake umesababisha vijana takribani 37,000 waliofaulu darasa la saba kukosa nafasi za kuendelea na sekondari kwa kipindi hiki cha miaka mitano..."
24 Machi 2005     
Sera ya Maendeleo ya Vijana Tanzania
"...Mathalani wakati hakuna mbunge hata mmoja aliyechini ya miaka 27, kuna wabunge 17 tu wenye umri kati ya miaka 27 na 35. Sera iseme wazi kwamba hakuna chombo cha kuwawakilisha vijana nchini - Hakuna baraza la vijana nchini. Hivyo inapokuja suala la kuchagua wawakilishi wa vijana katika michakato mbalimbali mfumo wa 'mimi namjua' hutumika..."
14 Januari 2005     
Concerned Students should reform UDSM politics
"...militant student organization USARF that was established by Yoweri Museveni and other activists like Walter Rodney, Issa Shivji and Horace Campbell. DUSO was banned in 1978 following the demonstration by students against the move by the members of parliament to hike their salaries while the country was in a deep economic crisis...."
5 Disemba 2004     
Bila baraza na sera ya vijana MKUKUTA utagonga ukuta
"...Vijana wengi wanazidi kuwa walalahoi. Kama unabisha nenda mitaani, waulize vijana-katika kila kumi, sita ni masikini kwa viwango vya kimataifa, wanne kati yao ajira kwao ni ndoto! Hivyo kizazi kipya kinapaswa kutwaa jukumu la kuleta maisha mpya...."

- - - MWISHO - - -


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl