lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Mengineyo
»Makala zingine
»Habari Mpya
»Matamko ya Chama
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
»Katuni
b.part
Barua Pepe
   
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Makala za Kitila A. K. Mkumbo

13 Aprili 2008     
Tumekubali kubaki mateka wa CCM?
"...KWA takriban wiki mbili sasa, nchi yetu imeendelea kugubikwa na habari kuhusu mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, uliofanyika Butiama, mkoani Mara. Katika kipindi chote cha mkutano huu wa CCM, waandishi wengi muhimu walivihama vituo vyao vya kazi Dar es Salaam wakaenda Butiama, kiasi cha kwashangaza hata wenye mkutano..."

20 Februari 2008     
Kuanguka kwa Lowassa tucheke au tuchekelee?
"...KAMA ilivyotarajiwa, kujiuzulu (wengine wanasema kususa) kwa Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu kulikofuatiwa na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri, kumepokelewa kwa hisia mchanganyiko. Ni wazi kuwa wananchi walio wengi wameonekana kufurahishwa kwa kuondoka Lowassa katika kiti cha uwaziri mkuu ..."

30 Januari 2008     
Kiteto tuanzishieni safari ya mabadiliko
"...KUNA imani kwamba Watanzania ni wepesi wa kusahau mambo makubwa ya kitaifa. Kuna imani pia kwamba Watanzania ni wepesi wa kukubali yaishe pale wanapoona jambo fulani walilokuwa wanalidai limekataliwa na serikali, hata kama wanajua kuwa msimamo wa serikali si sahihi..."

16 Januari 2008     
Tutaacha lini kumshangilia Kikwete kwa mafanikio hewa?
"...Nimekuwa nikitafakari uamuzi wa Rais Kikwete wa kumuachisha kazi Ballali na kujiuliza kama kweli Rais Kikwete anastahili au kustahiki sifa anazomwagiwa. Niseme wazi mwanzoni kabisa kuwa natilia shaka sana sifa ambazo Rais Kikwete anapewa; na niseme pia kwamba kwa maoni yangu tunamshangilia Kikwete kwa mafanikio hewa..."

28 Novemba 2007     
Kamati ya Madini ikajifunze kwa Hugo Chavez, Venezuela
"...Wapo wanachama wa CHADEMA kwa nia nzuri walipinga kushiriki kwa Zitto katika kamati hii kwa kuona kuwa kuteuliwa kwake ni janja ya Rais Jakaya Kikwete na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kujaribu kumziba mdomo baada ya kuinyima usingizi CCM na serikali yake kwa muda sasa. Kwa haraka haraka, ni rahisi kuona mantiki ya wale waliokuwa wanapinga ushiriki wa Zitto katika kamati hii..."

21 Novemba 2007     
Malecela alikwamisha utabiri wa Mwalimu Nyerere?
"...Tukio moja la aina yake ni ukweli kwamba CCM imeendelea kuwa chama pekee katika ulimwengu wa demokrasia bado kinachoendelea kuchagua viongozi wake kwa mtindo wa kikomunisti wa kura ya ndiyo au hapana. Haiyumkini pia kwamba wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hiki ambao wote ni watu wazima, tena wenye upeo wa juu kabisa wa kuelewa mambo, wanakaa siku mbili kwenye kikao kwa ajili ya kubariki majina ya wajumbe wa Kamati Kuu wote walioteuliwa na mtu mmoja..."

5 Septemba 2007     
Sumaye na CCM wametushtua
"...Hebu turejee tena maneno ya Sumaye. Katika mahojiano yaliyochapishwa katika Gazeti la Sunday Citizen la tarehe 26 Agosti 2007, Sumaye, pamoja na mambo mengine, alikaririwa akisema kuwa, ninamnukuu, “Nilikuwa kipofu kwa nini umaskini ulikuwa hauishi Tanzania na Afrika kwa ujumla, lakini sasa naweza kuelewa sababu za mateso yetu. Sumaye aliendelea kusema kuwa: “Wakati wa uongozi wangu, nilikuwa nashangaa kwa nini, pamoja na juhudi zote ambazo tulizifanya katika serikali pamoja na misaada kutoka kwa wafadhili, bado nchi yetu iliendelea kuwa maskini..."

22 Agosti 2007     
Tunahitaji akina Zitto 200 na akina Mudhihir 0 bungeni!
"...Mengi yamesemwa kuhusu hatua iliyochukuliwa na Bunge. Wapo waliolaani sana, ambao ndio wananchi walio wengi; wapo pia waliopongeza uamuzi wa Bunge na hawa ni wale wateule wachache ndani ya CCM wanaodhani wao pekee ndio wana akili, na sisi wengine hamnazo. Kwa upande wangu, naona kwamba yaliyompata Zitto ni matokeo ya mfumo wetu wa utawala uliojengwa na CCM tangu mfumo wa vyama vingi uanze..."

6 Juni 2007     
Wapinzani tafuteni kwanza itikadi na falsafa inayofanana
"Katika kujipambanua kiitikadi na kifalsafa, ni muhimu kwa upinzani kuchukua hatua ya kuwaelimisha wananchi wa kawaida ukweli kwamba kuna itikadi mbalimbali za kisiasa na pengine bora zaidi kuliko itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Hii ni hatua muhimu kwa sababu tangu nchi yetu ipate uhuru mwaka 1961, wananchi walio wengi hawajawahi kupata nafasi ya kujua uzuri wa itikadi zingine za kisiasa zaidi ya ile ya ujamaa na kujitegemea...."

30 Mei 2007     
Kwanini tunaogopa hata kuwanunia viongozi wetu?
"Kabla ya kuwalaumu viongozi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao, inabidi wananchi wajilaumu kwanza wao kwa kushindwa kuwafanya viongozi hao watekeleza wajibu wao. Kwa hiyo, kwa kuwachekea tu viongozi wetu bila kuwashinikiza kutekeleza wajibu hatuwasaidii, na wanaposhindwa tunapaswa kujilaumu zaidi sisi kuliko hata tunavyowalaumu wao..."

23 Mei 2007     
Tatizo la CCM si kukosa watu wenye uwezo wa kuongoza
"Uchaguzi wa mwaka 2005 ulionyesha kwamba Watanzania walikuwa wamechoshwa na utawala wa Rais Benjamin Mkapa, na kwamba walikuwa wana hamu ya mabadiliko katika uongozi wa kisiasa wa nchi yetu. Pili, uchaguzi ule ulionyesha pia kwamba Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa anatosha. Kutosha kwa Kikwete kulithibitishwa na ukubwa wa ushindi wa kura alizopata katika uchaguzi huo...."

2 Mei 2007     
Tutaendelea kuita koleo kijiko kikubwa hadi lini?
"KUNA tamaduni na imani zingine ifike mahala Watanzania tuziache. Imani kwamba mkubwa akikosea haambiwa amekosea ni imani mbovu na potofu. Kwamba mkubwa haambiwi ‘amechafua hewa’ bali shetani mbaya amepita, ni utamaduni uliopitwa na wakati..."

25 Aprili 2007     
Elimu kwetu ni mahitaji au matakwa?
"NI aibu kwamba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimefungwa kwa mara nyingine tena kwa sababu ya mgomo wa wanafunzi. Sote tunalazimika kuendelea kutafakari sababu na namna ya kumaliza migomo ya wanafunzi katika vyuo vyetu. Tukitafakari sababu za migomo hii, ni muhimu pia tujiulize swali; ‘hivi elimu kwetu ni mahitaji au matakwa?’..."

11 Aprili 2007     
Kura za kishindo zimewapa watawala kiburi
"WANASIASA na wafanyabiashara wana udhaifu mmoja mkubwa unaofanana; wote hupatwa na kiburi pale wanapotambua hawana mshindani. Mfanyabiashara anapogundua kuna mfanyabiashara mwenzake anafanya biashara kama yake, tena katika maeneo hayohayo, hujitahidi kutoa huduma nzuri kwa wateja wake, ili kuhakikisha kuwa hawamkimbii na kwamba anaongeza wateja zaidi..."

4 Aprili 2007     
Kikwete ni dereva mzuri ila gari analoendesha lilishakufa
"...Kama Kikwete aliota kuwapatia Watanzania maisha bora na kwamba angeutumia urais kama nyenzo ya kutimiza ndoto yake hii, basi inabidi ajipange upya. Bila kujipanga upya ni wazi kuwa Kikwete hatoweza kuitekeleza ndoto yake. Hii ni kwa sababu miezi 15 baada ya kuchaguliwa kuwa rais, bado hakuna dalili zozote za maana..."

28 Machi 2007     
Kikwete; tushike anayoyasema au anayoyatenda?
"...Kwa wanasiasa walio waadilifu, kuna kanuni tatu pia. Kwanza, mwanasiasa atawaambia wananchi wake kile ambacho amepanga kufanya na kwa nini anafikiri ni muhimu kufanya hicho kitu. Pili, atafanya kile alichowaambia wananchi wake kwamba atakifanya. Tatu, akishakukifanya, atawaambia kwamba amefanya kile alichofanya na kuonyesha mazao au matunda ya yale aliyoyafanya..."

29 Oktoba 2005     
Mbowe amejenga hoja, Ameeleweka, Tumpe Kura
"Wataalamu wa saikolojia ya siasa (political psychology) hugawa wapiga kura katika makundi makubwa manne. Kundi la kwanza linajumuisha wale watu wanaomchagua mgombea kwa kuwa mgombea huyo anatoka nao chama kimoja. Hawa kwao hoja au haiba ya mgombea sio muhimu; muhimu kwao ni kwamba mgombea ni kada mwenzao..."



lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl